Search This Blog

Saturday, May 14, 2011

TEVEZ AONDOKE KAMA HANA FURAHA-MANCINI


Kocha wa Manchesterb City Roberto Mancini amemwambia mshambuliaji wa timu Carlos Tevez hiyo acheze kwa kujituma kwa asilimia 100 au aondoke Eastlands.
Tevez ambaye aliomba kuondoka Man City earlier this season kabla hajabadili mawazo na kuamua kubaki, amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamishia huduma zake nchini Italia katika klabu ya Inter Milan.
Akiongea na vyombo vya habari Mancini amesema kama the Aegentian Striker hana amani ndani ya Man City basi aondoke, “Tevez ana mkataba wa miaka mitano hapa lakini kwa maoni kama mchezaji anataka kukaa hapa inabidi ajitume kwa 100% na awe na furaha lakini kama hana furaha na amani ni aondoke.”
Hata hivyo Carlos Tevez ambaye alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya bega, amepona na leo anatarajiwa kuanza katika mechi ya fainali ya kombe la FA dhidi ya Stoke City.

No comments:

Post a Comment