Search This Blog

Thursday, August 4, 2011

Vita , Amani na Kombe la Dunia.


Kikosi cha sasa cha Ethiopia...
Hakuna kinachovutia vyombo vya habari kama habari zenye zengwe ndani yake , hakuna , ni zengwe mwanzo mwisho . Chochote kinachohusu eneo linalofahamika kijiografia kama pembe ya Afrika kwa wiki chache zilizopita kimetawaliwa na ishu ya janga la njaa linaloikabili sehemu hiyo . Janga hili linasemekana kuwa kubwa kuliko yote yaliyowahi kuikumba Afrika kwa takribani miaka 60 iliyopita . Eneo la mashariki mwa Ethiopia lina wakazi wengi ambao wana asili ya kisomali na watu hawa wamejenga uhasama kama si utani wa soka ambao umekuwa upinzani mkubwa na wenyeji wao ambao ni waethiopia . Hili ni jambo geni kidogo na ilipofanyika ‘draw’ ya michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 upinzani huu ulichagizwa pale ambapo Ethiopia na Somalia walipojikuta wakikutana . Hakika wapangaji wa ratiba hiyo hawakuwa wanajua ni uhasama wa aina gani umefufuliwa kwa draw ile ya kuwaweka wasomali na waethiopia kwenye mchezo mmoja .

kikosi cha kale cha Ethiopia
Somalia si mpinzani mkubwa wa Ethiopia kwenye soka , wapinzani wa Ethiopia kwa miaka mingi wamekuwa Sudan , Uganda na hivi karibuni Rwanda. Ila wasilojua wengi ni takwimu isemayo kuwa Ethiopia haijawahi kuwafunga wapinzani wao toka mashariki mwa nchi yao Somalia tangu mwaka 2004 na waethiopia siku zote wamekuwa fasta kutoa sababu ya kutowafunga wasomali wakisema kuwa timu yao ( Ethiopia) imekuwa haina umoja na sio kwa sababu Somalia ni timu bora kuliko Ethiopia .



Kikosi cha sasa cha Somalia..

Timu ya taifa ya Ethiopia maarufu kama Waliyas iliwahi kutwaa ubingwa wa CECAFA CHALLENGE mwaka 2003 . Katika mafanikio hayo waliongozwa na Asrat Haile kocha mwenye mafanikio kuliko wote kwenye soka la nchini Ethiopia . Mwaka mmoja baada ya kutwaa ubingwa wa CECAFA Asrat aliondolewa kama kocha mkuu na kupewa jukumu la kuwa msaidizi wa kocha wa Kijerumani Johan Figge. Asrat aliweka wazi kuwa asingeweza kufanya kazi chini ya Mjerumani huyo na ‘beef’ hili lilihamia kwa wachezaji ambao wengi wao walichukua upande wa Asrat .
Katika kipindi cha ugomvi huu baina ya Asrat na Johan ikaja mechi dhidi ya Somali na athari zake zilionekana kwani Ethiopia walifungwa na hii ilikuwa ishu kubwa kwenye nchi zote mbili .


Kikosi cha kale cha Somalia
Somalia na Ethiopia wamepigana vita kuu mbili katika historia yao kwenye miaka 1964 na mwaka 1977 na kwa sababu hiyo wamekuwa na uhusiano mbaya kweli kweli . Miaka miwili baada ya Somalia kuwafunga Ethiopia wasomali waliingia kwenye vita mbaya ya wenyewe kwa wenyewe . Majeshi ya Ethiopia yalivuka mpaka wa Somalia na ugomvi baina ya nchi hizo mbili ukaibuka tena . Tangu mchezo wa mwisho ambao Somalia ilishinda timu hizi hazijakutana tena kwenye mechi ya soka na watakapokutana kwenye mechi ya kufuzu kombe la nyasi zitawaka moto .

1 comment:

  1. Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kila upande, Waethiopia walikimbilia Somalia na baada ya vita nchini Somalia wasomali walikimbilia Ethiopia, hapo ndipo watu wa nchi hizi mbili wakaanza kujuana lakini kwa wananchi tuu. Serikali zilibaki kutoaminiana kwa kila upande ingawaje kiongozi aliopo sasa Ethiopia Meles Zinawi aliishi Somalia kama mkimbizikwa miaka 11

    ReplyDelete