Mashabiki
wa Simba na Yanga kwenye miji ya Tunduma na Morogoro nao watapata fursa ya
kuburudika katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe
lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa
Mwaka mjini Tunduma na Kiwanja cha Ndege mjini Morogoro siku ya Jumapili
wikendi hii.
Mratibu
wa mabonanza hayo Lawrence Andrew, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka
bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani
maarufu kama fussball itapamba mabonanza hayo. Burudani mbalimbali pia
zitapamba bonanza litakalofanyika Tunduma zikiwemo burudani ya muziki kutoka
bendi ya High Class pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa
mkoani Mbeya.
Kwa
Mkoa wa Morogoro bendi maarufu mkoani humo ya Beacon Sound itatoa burudani
kabambe kwa mashabiki watakaojumuika kushiriki bonanza hilo huku wasanii wa
kundi maarufu la dansi GYT wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Andrew
pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile
kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa
kitambaa usoni itapamba mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa
mara ya kwanza kupitia Nani Mtani Jembe.
Kampeni
hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na
kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya
mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza
hayo yanalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani
Mtani Jembe ambayo ilizinduliwa Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima
ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni
hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga
kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila
timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga
wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa
timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea
namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi
milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni
shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro
Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema
baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo,
anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe
mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba
iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema
baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka
kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa
amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa
shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
Kwa
mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au
Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14,
mwaka huu.
Kwa
mujibu wa matokeo kama ilivyotangazwa kwenye https://cms.rasello.com/kili
tovuti maalum ya Nani Mtani Jembe timu ya Yanga inaongoza kwa kuwa na kiasi cha
shilingi 55,600,000 huku Simba ikiwa na shilingi 44,400,000 hii ikiwa ni baada
ya Simba kuongoza kwa takribani wiki mbili sasa hatimaye Yanga wamewapita.
No comments:
Post a Comment