Search This Blog

Friday, November 15, 2013

MAKALA: THAMANI YA JEZI YA TAIFA, NA UCHAGUZI WETU WA WACHEZAJI


Na Baraka Mbolembole

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza na timu ya
Taifa ya Kenya katika mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu baadae wiki ijayo. Kwa sasa timu hiyo ipo kambini pamoja na ile inayofahamika kama ' Future Young Taifa Stars', zikijiwinda na mchezo huo sambamba na michuano ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, Tusker Challenge Cup ambayo itapigwa baadae mwezi huu hadi mwanzoni mwa mwezi ujao nchini
Kenya.

Timu hizo mbili juzi zilicheza mchezo wa wao kwa wao na ile ' YoungTaifa Stars' kuitambia, Stars na kuichapa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Karume, zilipo ofisi za  shirikisho la soka nchini, TFF, na hatimaye jana kutangazwa rasmi kwa timu ya Taifa ambayo itacheza michuani ijayo ya Challenge.
  ILIPOTOKA STARS, INAPOKWENDA.....
Tanzania ilimaliza katika nafasi ya tatu katika kundi la kufuzu kwa
fainali za Brazil, wakiwa wamepata ushindi mara mbili na kufungwa maranne . Chini ya kocha Kim Poulsen timu hiyo ilitolewa katika harakati za kufuzu kwa AFCON 2013 na timu ya Msumbiji, na ilishika nafasi ya nne katika michuano iliyopita ya Challenge, 2012, nchini Uganda.

Makocha wa zamani wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo, na Mdenish, Jan Borge Poulsen walikuwa wakilaumiwa sana na mashabiki wa soka kwa kushindwa kuleta mabadiliko katika timu hiyo. Jukumu hilo akapewa KIM.

 KIM, aliamua kubadili mfumo wa kiuchezaji, kutoka ule wa kutumia nguvu na kuanza kutumia wachezaji wenye vipaji zaidi na wanaojituma.
Alitarajia mpango wake huo ungeweza kumpatia mafanikio, lakini
haukufanya kazi hata pale Stars ilipokabiliana na timu ya Taifa ya
Uganda katika kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani. Stars iliyotimia ilifungwa katika michezo yote miwili ya mtoano dhidi ya ' The Crannes' ambayo ilikuwa na mchezaji mmoja tu wa kikosi halisi cha nchi hiyo.

Mfumo huo mwanzoni haukuonekana kuwakera wengi, ila katika siku za karibuni umekuwa ukiwaudhi mashabiki wengi ambao wanaona jambo analofanya NI gumu kwa Tanzania na haliwezi kutoka matunda yoyote

Mabadiliko makubwa ambayo KIM, ameyafanya tangu mwezi, machi, 2012 alipokabidhiwa timu hiyo ni kumpandisha kiungo, Salum Abubakary ambaye hakupewa nafasi wakati wa utawala wa Maximo na Jan. Kuwa na majukumu ya kuinoa timu ya Taifa siyo kazi ya kuwa na moyo wa kubabaika. Wakati mwingine mwalimu unatakiwa kujenga imani kwa wachezaji vijana, pengine imani ya Kim kwa wachezaji vijana imekuwa ni sababu ya uwepo wake hadi sasa, ila hata Maximo na Jan walijaribui jambo hilo ila waliishia kupigiwa kelele za kuondoka, na wakaondoka wakliwa hawajafikia hata nusu ya matarajio yao.

 Huwa kuna ukiritimba mkubwa katika timu yetu ya Taifa. Kuna mapendekezo mengine yanakuwa katika hali ya haki na usawa, ila yapo mapendekezo mengine ya wachezaji huwa ni ya kipuuzi sana. Kujihusisha katika mambo hayo ni sawa na KIM kujiondoa mwenyewe katika taaluma ya ukocha.

Lakini pamoja na kuwa na kazi ya kuchagua wachezaji kama mwalimu, pia KIM, anatakiwa kuangalia anavyoweza kuisadia Tanzania kupiga hatua ya kiuchezaji ndani ya uwanja na si kupanda katika renki za FIFA ambazo wakati mwingine haziendani na uhalisia wa mchezo wetu.

KIM, amekuwa mtu wa mipango ambayo itakuwa muhimili wa kuwa na kikosi imara cha timu ya Taifa. Ili kupata wachezaji wanaoweza kuishawishi jamii imuamini, ila kama kocha ambaye anaweza kuwajibishwa jambo hilo linaweza kuwa hatari sana. Pamoja na kazi ya kuchagua wachezaji kama mwalimu, pia kazi ya kocha ni kuangalia mfumo wa uchezaji, mbinu na ufundi, na moja ya nguzo muhimu kama mwalimu pia ni kuweka umoja katika timu na hilo limekuwa likioneshwa na KIM.
    
 KIM, AMEFELI AU AMEFAULU?
Bila shaka hata KIM mwenyewe atakuwa anatambua kuwa kipindi cha yeye kuwa kocha wa timu hiyo kinaweza kuamuliwa na matokeo ya Nairobi, Kenya katika michuano ijayo ya Challenge. Watu wengi wamekubali kushindwa katika harakati za kufuzu kwa AFCON 2013, kushindwa kutwaa Challenge, 2012, kushindwa kufuzu au kumaliza nafasi ya pili kwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa kanda ya Afrika, kushindwa kufuzu kwa CHAN 2014, Ila sifikirii kama ataendelea kuwa mtu sahihi endapo atashindwa kufika walau fainali katika michuano ijayo ya Challenge. Timu bora hujijenga huku zikipiga hatua katika michuano ya kimataifa. Hivyo itakuwa haina maana kusema tunawaendeleza yosso wetu kama kina Salum huku wakishindwa hata kucheza fainali ya michuano ya ukanda wetu.
Tunatakiwa kupigania mataji katika kila michuano ya ukanda huu, huku tukiwa na lengo la kuwandeleza vijana wetu wenye vipaji katika timu ya taifa, hali ya mazoea ya ushindi huwa ni kitu kizuri. Iitazame Uganda, utawala wao wa soka la kanda ya CECAFA, umewafanya kuwa na timu kali na wamejaribu mara nne mfululizo kufuzu kwa michuano mikubwa ya Afrika na ile ya kidunia, ila hawakuwa na vitu vingine vya ziada. UDHAMINI, kama ambao upo nchini kwetu.
   LA KUJIULIZA....
 Je, Stars itajijenga kwa mfumo wa sasa ambao hata wachezaji wasio na nafasi katika klabu zao
huchaguliwa?. Inakuwaje kuwa na wachezaji zaidi ya 40 ambao kwa pamoja wana sifa za kuiwakilisha nchi?. Ndiyo tunao wachezaji wenye vipaji lakini hata Brazil haina rundo la wachezaji bora zaidi ya 40 kwa
wakati mmoja, ambao wanaweza kuiwakilisha timu yao ya Taifa. Kwa uwepo wa timu ya pili ya Taifa, KIM ameshindwa kuwa na mtazamo mzuri katika hili kwa kuwa wachezaji hao wengi ni vijana, ambao wangeweza kukua vizuri wakiwa timu za vijana ambako wangeweza kucheza mashindano na kupata uzoefu huko. Na, wapo ambao hawachezi katika klabu zao ila hupewa nafasi,.

Wachezaji kama Miraj Adam, Adam Ramadhani, Amri Kiemba, Haji Nu hu, ni baadhi ya wachezaji ambao kimsingi hawakuwa na sifa za kuitwa kikosini kwa sasa. Wapo chini ya utaratibu wa machaguo ya timu ya Taifa. Timu ya Taifa ni muhimu kuliko matakwa binafsi ya Mtu.
 Kim, anatakiwa kupewa nafasi ya mwisho sasa. Baada ya kutolewa katika AFCON, kushindwa kutwaa taji la Challenge, kushindwa walau kumaliza katika nafasi pili katika kundi la kufuzu kwa kombe la dunia, kushindwa kufuzu kwa CHAN, CHALLENGE YA NAIROBI, Iwe nafasi ya mwisho kwa KIM.


 TIMU YA TAIFA IMARA, LIGI IWE IMARA PIA
Kuitwa kwa mshambuliaji, Elius Maguli wa klabu ya Ruvu Shooting ni moja ya machaguo ambayo yalitarajiwa na wengi. Amefanikiwa kufunga mabao tisa katika duru la kwanza la ligi kuu, Pia uchaguzi wa mara nyingine wa Juma Luizio wa Mtibwa Sugar umekuwa ni sahihi kwa kuwa amefanikiwa kufunga mabao tisa katika ligi kuu iliyosimama.
Mshambuliaji wa Azam, John Bocco amekuwa na miezi isiyovutia,
ameshuka sana kiwango, pengine naye alistahili kuwa kundi la kina
Kiemba. Hasingeitwa, timu ya Taifa ni orodha ya wachezaji bora wa nchi katika wakati husika. Bocco ni kielelezo kingene kuwa KIM, hatakiwi kuwa na timu mbili za Taifa, bali kuhakikisha anakuwa na timu moja imara ya Taifa ambayo itajumuhisha wachezaji bora waliofanya vizuri katika ligi ya ndani ambayo ndiyo pekeeinayoweza kutoa wachezaji wa kikosi hicho, au wale wachezaji bora wanaopata nafasi katika klabu za ng'ambo na kufunya vizuri. Huku akihakikisha wachezaji vijana kama Aishi Munula wakipata nafasi ya kukua vizuri kiumri na kimchezo katika timu za vijana.

Ni kama kwa David De Gea, kipa namba moja wa Manchester United kwa misimu mitatu sasa ila hana nafasi katika timu ya Taifa ya Hispania kutoka na uwepo wa makipa Iker Cassilas, Victor Valdes, na Pepe Reina. De Gea, amebaki kuwa chaguo sahihi namba moja katika timu za taifa za vijana. Si, kila mchaji '  yosso' anaweza kuingia moja kwa moja katika timu ya Taifa na kufanya vizuri. Pele' ' Mfalme wa kandanda' duniani alianza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 16, na mwaka mmoja baadae akafunga mabao sita katika fainali za kombe la dunia akiwa na miaka 17.
Ila, bado tunawataza wachezaji kama Xavi Hernandez,. Andrea Pirlo, Frank Lampard, Steven Gerrard wakiwa nguzo kubwa ya timu zao za Taifa huku wakiwa juu ya miaka 33. Ila Ujerumani ina makinda wengi na hufanya vizuri, ila Kina Ozil Mesut, Sami Khedira, Jereome Boateng, Org Bardistuber, Marko Marin, Mario Gotze wameshatwaa taji la vijana la Ulaya, watakapo pevuka wanaweza kuvunja mwiko wa kuishia nusu fainali katika michuano ya kombe la dunia mara mbili na mara moja wakifungwa katika nusu fainali ya Euro.
 WACHEZAJI WETU WANAWAZA NINI?
Nafikiri kwa mchezaji ambaye hufikia kuitwa wa hadhi ya kimataifa, ni lazima ajitahidi kuonesha vitu tofauti katika uchezaji wake. Kila namba ya mchezo inapoongezeka kwa mchezaji kucheza mechi za kimataifa ni muhimu akijitambua kuwa anatakiwa kupiga hatua zaidi kiuchezaji, kiuzoefu, umakini, huku akiona fahali kuiwakilisha nchini yake katika michezo ya kimataifa. Wanatakiwa kuziheshimu timu zao na kuhakikisha kila mara wanacheza katika kiwango cha juu ili kulinda nafasi yake katika timu ya Taifa. Ni fahali kuchezea timu ya taifa, wajibu ni kitu muhimu na huanzia katika  moyo wa mtu mwenyewe, na si wa kulazimishwa.
 0714 08 43 08

2 comments:

  1. Nakubaliana na wewe kabisa, hivi kuwa Azam ni tayari upo timu ya Taifa?

    ReplyDelete
  2. Kila kocha ana vigezo vyake na mara nyingi inategemea na mfumo anaoutumia, partnership ya wachezaji mbalimbali n.k.
    Sina uhakika na qualifications zako lakini huwezi kutaja nani anafaa au hafai kuchaguliwa. Hata hao madogo inawezekana wapo wataoingia moja kwa moja ktk first 18, au wapo watakaobahatika kucheza kutokana na mfumo wa kocha.
    Sasa unataka kufananisha Spain na Stars ?? kufananisha professional players na hawa akina Javu ?Digea unajua ni just a matter of time kuingia kikosi cha spain.

    Naona kama unajichanganya pia kwani Kiemba ana tatizo gani ? Kama ni kukaa bench (believe kuna sababu) mbona Lampard amelikalia sana lakini ktk England anapeta ? Casilas kacheza mechi ngapi ?

    Waacheni hao madogo wapikwe, na siajabu kwa mara ya kwanza soon tutaanza kuona matunda.

    ReplyDelete