Mechi
ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16
mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji
tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.
83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 20,886,282.09.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25
ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.
Ni pesa mingi,japo bado pesa nyingi zaidi huishia kwa walinzi wa magetini wanaopenyesha watu kwenda kukaa majukwaa ambayo hawakustahili mfano unakuta mtu kalipia tiketi ya buku tatu (3000) unamkuta kaenda kukaa kwenye jukwaa la waliolipa 15000 au 20000 yaani VIP.Kila mtu anakimbilia VIP (japo hayupo tayari kulipia gharama za kukaa majukwaa hayo).
ReplyDeleteSina hakika kama wahusika (tff) hawalifahamu hili au wanalifumbia macho kama kawaida yetu.Matokeo ya tabia hii chafu ni baadhi ya majukwaa kujaa kuliko uwezo wake.Unakuta viti vya jukwaa husika hasa VIP vimejaa vyote na barabara za pembeni ambazo ni maalum kuwezesha watu kupita kwenda maliwatoni zimejaa zote kiasi inakuwa hakuna hata sehemu ya kuweka mguu ukapita kwa amani.Kwa maana nyingine ile mantiki ya mtu kununua tiketi VIP inakuwa haipo tena.
Tabia hii pia inaweza kuleta maafa kwa sababu uwanja kitaalam uwanja unakuwa na makadirio ya kitaalam yanayowezesha kumudu idadi iliyopo.Iwapo idadi hii inazidi kwa tabia hizi za kupenyeza watu,ni suala la muda kabla tu hatujasikia kitu kibaya zaidi kinatokea pale taifa(japo hatuombei itokee).
Ushauri wangu kwa wahusika ni kuwa waangalifu kwa kuwabaini na kuwachukulia hatua stahili walinzi wenye tabia hii chafu (nina hakika watakuwa ni washen*** wachache wanaofahamika!)ambayo mara nyingi hufanywa pindi kunapokuwa na mechi kubwa.
daa...! Ule umati wote mil 500 tu
ReplyDeleteHawa jamaa washachakachua ile mechi ilikuwa na zaidi ya watu 60000 ambao ndo uwezo wa uwanja.Kuna watu kibao walikosa viti vya kukaa na kulazimika kukaa kwenye njia na wengine wengi tu kusimama wakati mechi inaendelea.
ReplyDelete