Klabu ya Russia Anzhi Makhachkala kwa mara nyingine tena itabidi wacheze mechi zao nyumbani za ulaya nje ya uwanja wao kwa msimu ujao kutokana masuala ya ulinzi, shirikisho la soka UEFA limesema leo Jumatano.
"Jopo la dharura la UEFA lilikutana na kuamua kwamba kutokana usalama mdogo huko Dagestan na Caucasus Kaskazini, hakuna mashindano yoyote ya UEFA yatakayoruhusiwa kuchezwa katika eneo hilowakati wa msimu wa 2013/14 season," UEFA ilisema kupitia taarifa yake.
"Kwa maana hiyo, Anzhi Makhachkala wameombwa kuchagua uwanja mwingine wa kuchezea mechi zao za nyumbani kwa msimu wa 2013/14 kwa ajili ya UEFA Europa League."
Anzhi wametumia fedha nyingi kusajili wachezaji kama mcameroon Samuel Eto'o na kumuajiri kocha mdachi Guus Hiddink pia kumsajili mbrazili Willian kwa 35 million euros ($47 million).
Walimaliza kwenye nafasi ya 3 kwenye ligi ya Russia msimu uliopita, wakikosa nafasi ya kwenda kwenye Champions League.
Anzhi walicheza mechi zao za Europa League huko Moscow msimu uliopita kufuatia kifungo kama hichi kutokana kwa UEFA.
No comments:
Post a Comment