Beki
wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa
ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika
mwakani nchini Afrika Kusini.
Kocha
Kim Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa
kushoto amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni
mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini
kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala
ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Mechi
ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki
mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.
Wachezaji
wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally
Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo
(Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja
(Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).
Wengine
ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam),
Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum
Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na
Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).
Hatimaye sasa Kim Poulsen ameacha ubishi na kuanza kusikiliza ushauri na kuufanyia kazi..Angalia alipoteua Young Taifa Stars alimuacha Luhende na badala yake katika nafasi hiyo aliwaita Miraji Adam,Emily Mgeta,Waziri Salum na Samih Haji ambaye kwa muda mrefu hajacheza Azam.Vicent Barnabas hajawahi kucheza nafasi ya beki kwa muda wote aliocheza ligi kuu kuanzia 2005,na si aina ya wachezaji wanaoweza kubadilishwa kutoka ushambuliaji kwenda kwenye ulinzi kama ilivyokuwa akina Nsajigwa,Twaha Hamidu n.k.sidhani kama anao ubora wa kuwazidi mabeki wa asili wa pembeni kama Cholo na Juma Abdul.Pamoja na kasi yake lakini Kwa sasa umri wake ni mkubwa,kimo chake ni kifupi na ana tatizo la kuangalia zaidi chini wakati akiwa na mpira.
ReplyDeleteMrisho ngasa ni yanga sio simba.
ReplyDelete