Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar
Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya
Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya
Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati, baada ya kutoka
suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri
na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo
kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.
Wachezaji wa timu ya Simba pamoja na
kocha wao wakipiga picha pamoja na kombe lao walilolikabidhiwa leo
kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika michuano
ya Urafiki inayoandaliwa visiwani Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la Urafiki.
Wachezaji wa timu ya Azam FC nao wakisalimiana na viongozi mpira wa miguu kutoka Zanzibar pamoja na mgeni rasmi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa timu ya Simba wakimnyanyua juu juu golikipa wao Juma K. Juma baada ya kupangua penati mbili katika mchezo huo uliokuwa wa fainali katika michuano ya Urafiki. |
Ubao wa matangazo ukionyesha Simba 5 Azam FC 3 kwenye uwanja wa Taifa.
Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Simba
kutoka nchini Zambia Felix Sunzu akichuana vikali na beki wa timu ya
Azam FC katika mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao. |
Salum Kinje akimpongeza Felix Sunzu kwa kufutupia bao la kwanza la Simba |
No comments:
Post a Comment