Search This Blog

Saturday, July 14, 2012

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 0-2 ATLETICO - FULL TIME


DK. 5 - Mpira ndio unaanza na timu zote zinaonekana kumiliki mpira kwa zamu.

DK 10 - Mchezo bado umetulia timu zinaonekana kusomana, ubaoni kunasomeka Yanga 0-0 Atletico

DK. 15 - Yanga 0-0 Atletico 
DK 30 - Yanga 0-0 Atletico 

Mpira ni mapumziko na timu zimetoka sare tasa mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamzilizika. 

Kipindi kinaanza ndani ya dimba la taifa, Yanga 0-0 Atletico. 

dk. 62 - Jerry Tegete ambaye hakuwa na mchezo mzuri leo anatoka na anaingia Said Bahanuzi ambaye ni mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga, matokeo bado ni tasa - milango ya timu zote bado ni migumu.

DK. 68 - Nizar Khalfani anaingia na Rashid Gumbo anatoka.

DK. 70 - Zikiwa zimebaki dakika 20 kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa na mwamuzi, timu zote bado hazijaweza kuweka mpira kwenye nyavu. Mechi inaelekea kuisha sare hii kama mambo yataendelea kuwa hivi yalivyo.  

DK 81 - Goaaaaaaaaaaaaaaaaaal - Atletico ya Burundi inapata bao la kuongoza hapa zikiwa zimebaki dakika takribani tisa mchezo kuisha. 

DK. 89 - Atletico wanapata bao la pili hapa - beki za Yanga zinakatika kabisa hapa uwanjani. 
DK. 90 - Mpira unamalizika hapa uwanja wa taifa. Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wanaanza vibaya michuano hii kwa kufungwa mabao mawili kwa bila. Kwa mchezo mzima Atletico walionekana kumiliki sana mpira kuliko Yanga, na nafasi kadhaa walizotengeneza wamefanikiwa kuzitumia vizuri mbili na kupeleka kupata ushindi huu.

11 comments:

  1. shaffih kama umeamua kutoa live updates za mechi ya kagame cup basi usichague mechi . Mechi ya kwanza ulikuwa wapi?. Pia updates zinachelewa sana. Why?

    ReplyDelete
  2. Endeleeni Kununua MAGAZETI na kusifia usajili wenu.mpira unachezwa uwanjani kila mtu anaona.
    Mkufunzjr.

    ReplyDelete
  3. Ubovu wa Yanga maneno mengi kuliko vitendo! mpira hauchezwi kwa majina bali vipaji na ufundishaji wa makini. Kocha analipwa mshahara wa 25 millioni bado anafungwa du sijui nani atatolewa kafara!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vp nyie mnayemlipa kocha 5m leo mmeshinda ngapi tena na timu mbovu kabisa,shaffih acha unazi wa kitoto uwe unatoa update za simba pia

      Delete
  4. Tatzo la yanga wao ni wakali magazetini,,hiyo ndio dawa yao eti atletco kbonde..kwel lakin kibonde chenye maji ya betri kimewaunguza..uchaguz ushaingia doa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakali wa uwanjani leo mmekuwa kimya

      Delete
  5. MIMI NILIJUA TU ITAKUWA HIVI. NGOMA IKIVUMA SANA MWISHOWE UPASUKA.
    KUNA BLOG MOJA INAONGOZA SANA KWA KUWASIFIA YANGA, SIJUI LEO WATAANDIKA NINI.
    KELELE NYINGI MPIRA HAKUNA

    ReplyDelete
  6. yanga siku zote ni vibonde

    ReplyDelete
  7. Msituingilie timu yetu nyinyi mnatimu yenu tuacheni wenyewe tuganye uchaguzi muone kazi itakavyoanza kwn ss hv hatuna uongozi Yangaa daima mbele nyuma mwiko.

    ReplyDelete
  8. kaka shafiih naona kazi tuliyokupa imekushinda,vipi yule jamaa yetu wa HUU NI UZALENDO? mbona hatujamuona naomba sana kila yanga inapocheza,anatupa burudani sana

    ReplyDelete
  9. Naungana na mdau wangu hapo juu@babu hiyo blog ilikua inasema YANGA imekamilika anaiita BARCELONA ya Bongo... Daah..

    ReplyDelete