Mshindi huyo wa mara wa tuzo ya Ballon d'Or aliingia kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza cha Barca mwaka 2004, mwaka mmoja baada ya Dinho kuwasili Nou Camp akitokea Paris Saint-Germain.
Huu ni wakati Messi anasema hatokuja kuusahau kwenye maisha na anakiri ukarimu wa Ronaldinho pamoja na kuwa staa mkubwa kumliko ulimfanya azoee kwa haraka maisha ya kikosi cha wakubwa cha Barca.
"Siku zote nimekuwa nikisema, siku tu nilipoingia chumba cha kubadilishia nguo Ronaldinho na wenzie Deco, Sylvinho na [Thiago] Motta walikaniribisha na kunipa baadhi ya vifaa, lakini zaidi ni Ronaldinho ambaye pia alinifundisha vitu vingi uwanjani na nje ya dimba," Messi aliiambia Barca TV. "Ulikuwa ni msaada mkubwa. Ni vigumu kuenda kwenye timu ya mastaa kama Ronaldinho na kupata ukarimu kama wake. Alifanya kila kitu kikawa rahisi kwangu. Nilikuwa na bahati kuwa karibu nae na kushea vitu vingi.
"Ninaweza kusema Ron ni mtu mzuri sana na hicho ndio kitu muhimu."
Ronaldinho aliiwezesha Barca kubeba makombe mawili ya Liga na Champions League wakati wa miaka yake mitano aliyoitumikia klabu hiyo ya Camp Nou na Messi anaamini kiungo huyo mwenye miaka 33 ana mchango mkubwa kwa mafanikio aliyonayo sasa.
"Ronaldinho ndio mtu aliyeleta mabadiliko makubwa kwenye klabu hii," anasema. "Klabu ilikuwa inapitia wakati mmoja m'baya sana lakini hali hiyo ilibadilika mara tu alipowasili. Msimu wake wa kwanza hatukushinda chochote lakini watu walimpenda sana. Baadae yakaja mataji na akawapa furaha watu wengi sana.
"Sio mimi tu naamini Barcelona pia kama klabu haipaswi kuja kusahau mchango wake kwa vitu alivyoifanyia klabu hii."
No comments:
Post a Comment