Leo Jumamosi tarehe 13, July: Tanzania itapambana na Uganda kwenye uwanja wa taifa katika mchezo wa kugombea nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza kwenye ligi za ndani.
Uganda Cranes ilitua Bongo wakitokea kwao siku ya alhamisi. Kikosi cha wachezaji 18 na kufikia kwenye hotel ya Sapphire iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam wakionekana kuwa kwenye hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa leo katika dimba la uwanja wa taifa unaoweza kubeba mashabiki zaidi ya 55,000.
Uganda wanatarajiwa kuchezesha wachezaji wengi wapya kwenye hatua hii ya kimataifa. Ukimuacha mlinzi Dennis Iguma na kiungo Wasswa Mawanda, ambao walicheza dakika zote 90 kwenye mchezo wa kugombea kwenda Brazil 2014 dhidi ya Liberia na Angola, wachezaji wote waliobakia bado hawajaonja utamu wa soka la kimatiafa.
Hakuna beki wa kushoto asilia kwenye kikosi hiki cha Micho, ukizingatia mchezaji aliyeitwa kuja kucheza kwenye nafasi hiyo Habib Kavuma, aliondolewa kikosini baada ya kugundulika kwamba alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo wa 2011 CHAN dhidi ya Gabon. Hili linamuacha Micho Akibakiwa na mbadala Yusuf Mukisa, beki wa kulia ambaye hujaribu kucheza nafasi hiyo pia.
Wachezaji wengine ambao wana uzoefu kidogo na michuano ya CHAN ni Ayubu Kisaliita, Patrick Edema, Tonny Odur Hamuza Muwonge, ambao walicheza kwenye michuano ya CHAN iliyofanyika Khartoum, Sudan.
Kutokana kuwa ugenini - Micho anategemewa kuipanga timu yake huku akicheza mchezo wa kuzuia sana na kushambulia kwa kushtukiza. Uganda wanaweza kuanza kwa mfumo wa 4-2-1-3, baadae wakibadilika kuja 4-3-3 na 4-4-2 kadri muda unavyozidi kusogea.
MCHEZAJI WA KUCHUNGWA: Dennis Iguma
Dennis Iguma ameimarika sana kwenye kiwango chake, kujiamini kwake na namna anavyojua kucheza kitimu. Mchezaji huyu ambaye alitumia utoto wake kupata mafundisho ya soka kupita chuo cha soka cha Entebbe, anaweza kucheza popote uwanjani kwa kiwango kile kile anachocheza kwenye nafasi yake ya kawaida.
Iguma, kwa sasa anaichezea klabu ya Sports Club Victoria University anategemewa kuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Stars wakiongozwa na Canavaro na Yondani.
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemrudisha kikosini beki wa kulia wa Yanga, David Luhende akitoa picha kwamba Shomary Kapombe beki halisi wa kulia atahamia upande wa kushoto. Hii inakuja baada kumpa mapumziko Nyoni ambaye alicheza ovyo kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Morocco na Ivory Coast.
Huku Uganda ikiwa ndio timu iliyo juu kisoka kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, kocha wa Tanzania alizungumza na kusema yafuatayo."Utakuwa mchezo mgumu sana kwetu kwa sababu Uganda ni timu nzuri; tumekuwa hatuchezi vizuri sana dhidi yao katika mechi za hivi karibuni."
Wakiwaondoa washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu, ambao wanacheza TP Mazembe ya DR Congo, Taifa Stars itakuwa na wachezaji saba ambao walicheza kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia 2014.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Simba amekuwa na kiwango kizuri sana kuanzia msimu uliopita kwa Timu yake ya klabu na sasa kwenye timu ya taifa. Ana akili ya mpira, anatuliza mashambulizi na kupeleka mashambulizi kwa adui pamoja kuwatengenezea nafasi wenzie. Ikiwa atacheza kwenye kiwango chake cha juu basi Uganda watapata taabu sana kumchunga Kiemba asiweze kuwadhuru.
TIMU ZINAZOWEZA KUANZA
CRANES XI (4-2-1-3):
Hamuza Muwonge (GK)
Nicolas Wadada - Savio Kabugo - Richard Kasagga - Yusuf Mukisa
Hassan Wasswa (Captain) -Dennis Iguma
Joseph Mpande
Tonny Odur -Patrick Edema - Ronald Muganga
TANZANIA XI (4-3-3)
Juma Kaseja (GK)- Captain
Shomari Kapombe - Yondan - Nadir 'Canavaro' Haroub - David Luhende
Sure Boy - Frank Domayo
Mwinyi Kazimoto
Mrisho Ngassa-John Bocco - Amri Kiemba
JE WAJUA ?
- Mpaka kufikia 12th July 2013, Uganda inashika nafasi ya 80 katika listi ya timu bora duniani ya FIFA - wakati Tanzania ikishika nafasi ya 121 na pointi 271.
- Uganda Cranes ilifuzu kucheza 2011 CHAN Championships jijini Khartoum, Sudan kufuatia kuifunga Tanzania nyumbani na ugenini.
- Uganda ilifunga goli moja katika CHAN iliyopita iliyofanyika Sudan. Ibrahim Saddam Juma alifunga goli dakika ya 77 dhidi ya Gabon.
- Kocha wa Uganda, atakuwa anaiongoza UG kwa mara ya nne tangu amrithi Bobby, ameshacheza dhidi ya Libya katika mechi ya kirafiki na kufungwa 3-0, akaja kushinda 1-0 na 2-1 dhidi ya Liberia na Angola katika mechi za kufuzu kombe la dunia 2014.
Tanzania iliwahi kushirikia michuano hii wakati tu ilipoanzishwa na kufanyika nchini Ivory Coast.
UTABIRI WETU
Tanzania 2-1 Uganda
Wewe una utabiri gani?
tanzania 1 - 1 uganda
ReplyDelete3-1,ushindi kwa tz
ReplyDeletekabla ya mechi 1-1 ,baada ya mechi uganda 1 tanzania yai.
ReplyDeletekwa wabrazil ukicheza nyumbani unaaminiwa kuliko wanje ya nyumbani...Uganda 2-1 Tanzania.
ReplyDelete