Akisajiliwa kwa kiasi cha £7m wakati wa dirisha kubwa la usajili msimu uliopita, wengi walidhani Aston Villa wamelipa fedha nyingi kwa mshambuliaji huyo wa Kibelgiji, lakini Banteke amethibitisha thamani yake baada ya kufunga mabao 19 katika premier league - 14 kati ya hayo ameyafunga ndani ya miezi 5 ya mwaka 2013, mengi kuliko mchezaji yoyte wa premier league.
Aston Villa tayari wameshesema kwamba Benteke ataondoka kwenye klabu hiyo ikiwa tu watapata fedha inayostahili, ambayo inatajwa kuwa ni zaidi ya £20m. Umuhimu wa Benteke kwa Villa sio kitu cha kushangaza kwa kuwa mchezaji huyo alifunga asilimia 40 ya mabao yote ya Villa msimu uliopita na kuwasaidia wasishuke daraja.
Timu zinazoripotiwa kuvutiwa na kumsajili Benteke ni Chelsea na Tottenham, ambao wote wanataka kuboresha safu zao za ushambuliaji kabla ya msimu mpya.
Hatma ya Torres na Demba Ba ndani ya Chelsea haijaeleweka huku tetesi zikisema wanaweza wakaondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuhangaika kucheza kwenye kiwango kwa muda mrefu, lakini huku Lukaku akirejea darajani akitokea West Brom alipokuwa kwa mkopo - ni kweli Benteke anahitajika ndani ya Stamford Bridge?
Wabelgiji hawa wawili kila siku wamekuwa wakifananishwa wakiwa wanagombea nafasi ya kucheza kama mashambuliaji kwenye timu y taifa, lakini ni vigumu sana kuamua yupi bora zaidi ya mwenzake.
Ukijaji kwa kupitia msimu uliopita, Benteke alimfunika Lukaku kwenye ligi kwa mabao 19 dhidi ya 17 na alikuwa mshambuliaji namba moja kwenye timu ya taifa wakati wote wa michuano ya kugombea kufuzu kucheza kombe la dunia. Lukaku ingawa alianza michezo kadhaa.
TAKWIMU ZINASEMAJE KUHUSU WACHEZAJI HAWA WAWILI
TAKWIMU ZINASEMAJE KUHUSU WACHEZAJI HAWA WAWILI
Lukaku aliweza kufunga goli kila baada ya dakika 118 ukilinganisha na Benteke ambaye aliweza kufunga goli kila baada ya dakika 149. Lukaku pia aliweza kupiga mashuti mengi golini - yaliyolenga lango na yaliyotoka nje (47 and 34), huku mashuti yaliyolenga lango akipiga moja kila baada ya dakika 43 wakati mashabiki wa Villa iliwalazimu kusubiri dakika 66 kuona shuti la Benteke likilenga lango - nii kwa kiasi inaonyesha namna watu hawa wawili wanavyotofautiana.
Lukaku anaweza kwenda pembeni wakati wa mashambulizi jambo ambalo litaipa uhuru nafasi ya kiungo - labda kumpa uhuru mtu kama Lampard kuingia ndani ya box - na hili linaweza kuonekana wakati akiwa na West Brom ambapo aliweza kupiga krosi 58. Benteke pia anaweza kufanya hivi, lakini siokwa kiasi kikubwa kama Lukaku - msimu uliopita aliweza kupiga krosi 11 tu kuingia ndani ya box.
Tottenham wanakuja kuanza kumtaka Benteke baada ya kumkosa mshambuliaji David Villa wakiwa wanamtafuta mfungaji halisi na sio kumtegemea Gareth Bale peke yake - wakiwa na washambuliaji wawili tu halisi ndani ya kikosi.
Jermaine Defoe alianza vizuri msimu uliopita lakini alifunga bao 1 tu ndani ya miezi 5 ya mwaka 2013, wakati Adebayor ni kivuli cha mchezaji aliyekuwa Spurs kwa mkopo kabla ya kusajiliwa moja kwa moja. Mtogo huyo alifunga mabao 17 na kutoa assists 11 katika msimu wa 2011/12, wakati kwenye msimu uliopita alifunga mabao 5 na kutoa assist 1.
Kukosekana kwa mabao kutoka kwa washambuliaji msimu uliopita kulipelekea Tottenham kukosa nafasi kwenye Champions League, kitu ambacho Benteke angeweza kuwasaidia. Mchezaji huyo wa Villa alikuwa na wastani wa 26% kutumia nafasi za kufunga nyingi kuliko Adebayor aliyekuwa na wastani wa asilimia 17.
Wakati Christian Benteke akiwa amewavutia watu wengi kwenye Premier League mpaka sasa, mashaka juu yake yataendelea kuwepo mpaka pale atakapoendeleza mauaji yake ndani ya msimu ujao na kuthibitisha hakubahatisha msimu uliopita.
Huku Lukaku akirejea na wakiwa fedha za kutumia, Chelsea wataongeza mshambuliaji mwingine kwenye kipindi hiki cha kiangazi. Tottenham nao wanaweza wakawa chaguo sahihi kabisa kwa Benteke ambaye atakuwa akicheza katikati ya mawinga Bale na Lennon ambao kwa hakika watamsaidia sana kung'ara kuliko alivyokuwa Villa lakini hilo litatokea ikiwa tu watalipa fedha ambayo Villa wanaitaka.
No comments:
Post a Comment