Kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil amezungumza na kusema alikuwa akitumia masaa mengi kujifunza mbinu za soka kiungo wa zamani wa timu hiyo Zinedine Zidane kupitia mtandao wa YouTube
Mchezaji huyo wa kijerumani ambaye mbinu zake na ufundi uwanjani umekuwa ukifananishwa na Zidane kwa kiasi fulani amesema kwamba mbinu zake nyingi za soka amejifunza kupitia kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa.
"Nilimuona mara ya kwanza Zizou [Zidane] katika World Cup nchini France, mwaka '98," anaelezea kiungo huyo mwenye miaka 24 katika mahojiano yake na Sport. "Kutokea wakati ule niliendelea kumfuatilia kupitia video zake akiichezea Madrid au Ufaransa.
"Mara nilipoona akifanya jambo jipya nilikuwa naenda uwanjani na kuiga, mara zote nilikuwa nafungua youtube kisha natafuta video zake mpya kujifunza zaidi."
Ozil atapata nafasi ya kufanya kazi kwa ukaribu kabisa na shujaa wake Zidane msimu ujao, baada ya mkurugenzi huyo wa soka wa Madrid kuthibitishwa kuwa kocha msaidizi wa Carlo Ancelotti.

noma sana
ReplyDelete