Mmiliki wa klabu ya Nigeria iliyofungwa mabao 67-0 katika mechi muhimu ameamua rasm kuachana na timu hiyo kwa kuivunja.
Bubayaro walifungwa na Police Machine, ambao walikuwa wanahangakia kupata nafasi ya kupanda daraja kutoka kwenye ligi ya daraja la nne nchini Nigeria.
Wapinzani wa Machine kwenye kupata nafasi ya kupanda Plateau United Feeder wao walishinda mechi yao dhidi ya Akruba kwa mabao 79-0.
Mamlaka za soka nchini Nigeria zimezisimamisha klabu zote nne zilizohusika katika mechi hizo mbili.
Police Machine walihitaji ushindi ili wawazidi Plateau United Feeder, lakini matokeo ya mwisho yaliwapa nafasi Plateau kupanda daraja baada ya kuwa na tofauti kubwa ya mabao.
Feeder ilifunga mabao 72 kati ya 79 ndani ya kipindi cha pili, wakati Machine walifunga mabao 61 baada ya mapumziko.
Mmiliki wa Bubayaro Shuaibu-Gara Ahmed Gombe, ambaye alikuwa Lagos wakati timu yake ikichezwa sehemu nyingine, alisema kwamba alitoa amri ya timu kutocheza mechi hiyo lakini amri yake ikadharuliwa na viongozi wa timu.
"Mara tu niliposikia taarifa za matokeo niliamua kuivunja timu.
"Nimeandika ombi kwa Polisi wa hapa Bauchi kuchunguza suala hili la asibu kwa soka la Nigeria na kuwakamata wote watakoku wawamehusika."
Pia inasemekana kwamba jaribio la polisi kuwakamata wachezaji baada ya mchezo wa Bubayaro lilishindikana baada ya maofisa wa timu na wachezaji kupotea mara tu baada ya filimbi ya mwisho.
Baadhi ya watu waliodhuria mechi hiyo wanasema kwamba kulikuwepo na matukio kama maamuzi ya kutatanisha, kuongezwa kwa dakika za mchezo bila sababu, maofisa wa timu ndio wakirudisha mipira kwa haraka baada ya mabao kufungwa badala ya watoto waokota mipira.
Mwandishi wa habari ambaye alishuhudia mchezo kati ya Bubayaro dhidi ya Police huku akiomba jina lake lisitajwa aliongea na BBC na kusema: "Wakati wa kipindi cha pili, tulianza kushuhudia mabao ya ajabu ajabu ya kujifunga, huku makipa wakicheza ovyo kabisa.
"Feeders walifunga kila mara. Maofisa wa timu wakageuka waokota mipira, badala ya kutoa mpira ulioingia kwenye nyavu wakawa wanaingiza mipira mingine uwanjani na mchezo ukaendelea hivyo .
"Kuna baadhi ya watu walikuwa wakiongea na simu kisha kuwataarifu maofisa waliopo kwenye uwanja mwingine kuhusu kinachoendelea pale uwanjani."
No comments:
Post a Comment