Search This Blog

Monday, March 10, 2014

VIDEO: HIVI NDIVYO MIKWAJU YA PENATI BAINA YA YANGA DHIDI YA AL AHLY ILIVYOKUWA

7 comments:

  1. Yanga wamejitahidi sana,pengine tatizo kubwa lilikuwa kuteua wapiga penati hasa wafungaji wa penati.Al Ahly walijiandaa vya kutosha kwa kutenga session ya mazoezi ya penati na bado walikosa penati mbili.Oscar hajawahi kuwa mpiga penati katika timu zote alizopitia ikiwemo Toto.Moro United na Ruvu Shooting, inaonekana alifanya vizuri katika mazoezi ya kupiga penati.Hata hivyo nje walikuwepo wapiga penati wazuri kama Nizar na Juma Abdul.Aidha kukosekana kwa Niyonzima nako kulichangia upungufu katika wapiga penatiMechi za aina hii zinahitaji ujanja wa hali ya juu katika kuandaa wapiga penati na kufanya subs za wapiga penati.Nafikiri next time watajiandaa katika maeneo yote

    ReplyDelete
  2. Wewe Bahanuzi kajifunze kupiga penati acha ushamba.Penati zinapigwa kwa kutumia akili (hata ikitoka nje unaweza kuona malengo ya mpigaji yalikuwa yapi)siyo miguvu kama unavyofikiria.

    ReplyDelete
  3. Dida alifanya kazi yake vizuri sana simlaumu kabisa.

    ReplyDelete
  4. Yanga wamejitahidi nafikiri kilichotokea ni makosa ya kiufundi na kimbinu katika benchi la ufundi,kwani viongozi na wachezaji wamewajibika kadri ya uwezo wao.Ni dhahiri Yanga hawakujipanga vizuri kwa penati,pengine walikuwa na uhakika wa kushinda ndani ya dakika 90 au kulinda ushindi wa Dar es salaam,vinginevyo hii ilikuwa nafasi yao nzuri zaidi kuwaondoa waarabu.Katika mechi ya aina hii lazima uwe makini na jinsi unavyowatumia wachezaji wenye uwezo wa kufunga penati kama vile Kiiza.Unapowaanzisha lazima uwe na uhakika watamaliza mechi ya aina hii,vinginevyo aingie kama sub..Lakini pia Juma Abdul na Nizar ni wazuri kwenye penati,hivyo ilibidi wawe sub za kuelekea kwenye penati.Oscar na Bahanuzi sio wapigaji penati wa uhakika hasa kwa mechi ya aina hii,Nafikiri sub ya Bahanuzi haikuwa sahihi na badala yake alipaswa kuingia Nizar au Tegete

    ReplyDelete
  5. Jamani hivi huyu kocha wa yanga alimtoa Mrisho Ngassa wakati aliona mwenendo wa mpira ni matuta au moja ishinde alikuwa na maana gani, Bahanuzi yuko benchi muda mrefu aliingia kwa kisingizio gani, Diego kiiza yupo wapi mimi naona wapigaji wetu wa penalty walionyesha kutoshinda kwa hivyo tumejitoa wenyewe hapo. Pia kumuomba mungu kwa waarabu kumewasaidia sana.

    ReplyDelete
  6. Wakati wa mikwaju ya penati Kaseja alikuwa muhimu kuwa golini

    ReplyDelete
  7. Bahanuz anajua sana kupiga penati. Ndo maana kwenye mech moja kati ya simba na yanga, matokeo yalikua moja kwa moja na goli la yanga lilifungwa na bahanuz kwa penati. Walikuwepo wote hao wanaotajwa but kocha akamchagua bahanuz. Kukosa penat wanakosa hata kina cristiano, baggio, messi. Hata ukiangalia penati yake alpga vizur, alimuamisha kipa na alpiga kwa nguvu. Sema alikosea vipimo. Tatzo la bahanuz amepoteza hal ya kujiamin kutokana na kutopewa nafas mara kwa mara. Pia sikuona sabab ya kiiza kutolewa. May b kocha hafaham uwezo wa kiiza kwenye penat, lakin hata mkwasa angemwambia. Yote kwa yote. Tunawasubir mashujaa wetu. Kikos kispanguliwe, mwakan naona nafas ya kufanya vzur zaid!

    ReplyDelete