Search This Blog

Friday, May 25, 2012

HISTORIA - FC BAYERN MUNICH NI TIMU YA WAGENI WALIOZAMIA MUNICH - TSV 1860 MUNICH NDIO WAKONGWE NA WAZAWA WA MUNICH




Katika kipindi hiki chote ambacho nimekaa hapa jijini Munich Ujerumani, nimepata kugundua vitu kadhaa vinavyozihusu klabu pinzani za jiji hili FC Bayern Munich na TSV 1860 Munchen.
Hizi ni klabu mbili ambazo zote zipo katika jiji moja na zinafanana kidogo na timu zetu pinzani za Simba na Yanga - Bayern Munich na 1860 Munich na zenyewe zina upinzani mkubwa sana na zote zinatumia kiwanja cha Allianz Arena kuchezea mechi za nyumbani lakini pia klabu hizi mbili zipo katika eneo moja ndani ya jiji la Munich - Umbali wa kutoka makao makuu ya Bayern mpaka 1860 Munich ni dakika 5 kwa kutembea.

Kihistoria TSV 1860 Munich ndio klabu ya kwanza kuanzishwa, ilianzishwa na mabavaria wenyewe miaka 152 iliyopita. Ilikuwa ndio klabu ya kwanza jijini Munich kupata mafanikio ya kucheza ligi kuu ya Ujerumani. Miaka ikasonga baada ya mbele mpaka ilipofika mwaka 1900, baadhi ya wageni kutoka nje ya jiji la Munich wakaamua kujiondoa kutoka kwenye klabu ile kutokana na kuona kwamba Mabavariani ambao ndio wenye timu kiasili hawawapi nafasi ya kutosha hivyo wakaamua kuunda klabu ya FC Bayern Munich.

Baasi wageni wakachanganyikana na wazawa kiasi na kuanza kuisimamisha FC Bayern Munich ambayo ilikuja na kuwazidi wapinzani wao 1860 Munich na kuwa klabu ya kwanza kutoka Munich kubeba kombe la ligi kuu ya Ujerumani.

Lakini pamoja na kwamba Bayern ndio timu yenye mafanikio makubwa kiuchumi na kisoka lakini bado TSV 1860 Munich wanachuana kwa kuwa na mashabiki wengi na Bayern ndani ya jiji hili la Mabavariani.

Hii ndio historia fupi na utofauti wa vilabu hivi viwili.

No comments:

Post a Comment