Na Oscar Oscar Jr.
0789-784858
Siwezi kushangaa siku moja nikiamka asubuhi na kusikia taarifa kwenye
vyombo vya habari kuwa, wamiliki wa timu ya Azam wameamua kununua Ndege yao
kwa lengo la kurahisisha Usafiri wa kwenda mikoani kucheza michezo yao
ya ligi kuu na ile ya barani Afrika ambayo timu hiyo imekuwa ikishiriki
kwa msimu wa pili sasa mfululizo.
Kila nchi duniani ina tamaduni zake na moja ya tamaduni za kitanzania ni
kushirikiana kwenye matukio muhimu ya kijamii.
Watanzania pamoja na
tofauti zao za dini, kabila, kipato daima wamekuwa pamoja kwenye mambo ya
kijamii kama vile misiba.harusi n.k Hata kama utakuwa na pesa kiasi
gani, kama huna tabia ya kushiriki na wenzako kwenye mambo ya
kijamii, siku yakikukuta utaona cha mtema kuni! Hii inatuonyesha kuwa
ushiriki na mahusiano mazuri kwenye jamii yako ni muhimu kuliko vikapu
vya pesa ulizonazo.
Klabu ya Azam ilianzishwa mwaka 2007 na kufanikiwa kucheza ligi kuu
msimu wa 2008/2009 kwa mara ya kwanza na kumaliza kwenye nafasi ya
8. Msimu wa 2009/2010 ilifanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya 3 huku
wakiweka histori ya kumnunua mshambuluaji wa klabu ya Yanga Mrisho
Ngassa kwa mamilioni ya pesa za Kitanzania. Azam waliweza kumsajili
kiungo wa Rwanda marehemu Patrick Mafisango, Kally Ongala, Jabir
Azizi, Ramadhani Chombo Redondo na mastaa kibao na hapa ndipo walipoanza
kuteka taratibu hisia za watanzania kama timu itakayoleta mapinduzi ya
soka nchini.
Watanzania baada ya kuona timu ya Azam inakuja na mbinu ambazo
zinaendana na soka la kisasa, wengi wakaamini kuwa hii ndiyo timu ya
kuishabikia. Azam wamejenga uwanja wao, wana timu bora ya vijana, wana
hosteli za wachezaji wao na mambo mengi mazuri lakini, hawana mashabiki!
Hata wale wachache ambao huwa wanaonekana timu hiyo ikicheza wanapiga
piga ngoma ni kama mashabiki bandia tu.Tayari Azam wamefanikiwa mara 2
mfululizo kucheza mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika, kwa
timu iliyoanzishwa mwaka 2007 haya ni mafanikio.
Watanzania wengi sana wanaipenda timu ya Azam lakini, wanashindwa
kujiweka wazi kutokana na namna timu hiyo inavyoendeshwa.Uendeshwaji wa
Azam fc haujampa nafasi mwananchi kushiriki na hii inatokana na timu
hiyo kujiweza kifedha. Azam wanasahau kuwa timu tajiri kama Real
Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester United na nyingine
kibao, mafanikio yao yamechangiwa zaidi na mashabiki lukuki wanaonunua
bidhaa za timu hizo na kuingia uwanjani kila mwishoni mwa wiki.
Shabiki duniani kote ni mchezaji wa 12 na ndiyo maana klabu kama ya
Bayern Munich ya nchini Ujerumani hairuhusu mchezaji wake yoyote kuitumia
jezi namba 12 kwa sababu wanaamini jezi hiyo inavaliwa na washabiki wao
wanaokuja kuitazama timu kwenye kila mechi wanayocheza.
Azam FC ni lazima wawape nafasi mashabiki ya kuwa sehemu ya timu
yao, kuna uwezekano wakafanya kila kitu ila kukosa mashabiki, itaendelea
kuwagharimu kila siku. Kwa kutumia kigezo cha mapato ya mlangoni
tu, unaweza kugundua kuwa huenda klabu Yanga ndiyo inaongoza kwa idadi
kubwa ya mashabiki huku ikifuatiwa na klabu ya Simba kwa karibu
sana. Mbeya city wanaweza kuwa nafasi ya 3 na Coastal Union kushika
nafasi ya 4. Azam fc hamjifunzi tu?
Klabu za Simba na Yanga hapa nchini,zinamashabiki wengi sana na hali hii
inatokana na sababu nyingi,chache kati ya hizo ni ukongwe wa vilabu
hivyo na mafanikio makubwa waliyoyapata kwenye ligi kuu nchini na
mashindano mbalimbali ya Afrika Mashariki na kati.Ingawa timu za Coastal
Union toka jiji la Tanga,Tukuyu Stars toka jiji la Mbeya na Mtibwa
sugar toka Morogoro nazo kwa nyakati tofauti zimewahi kutwaa Ubingwa wa
ligi kuu lakini ni wazi kuwa,Simba na Yanga ndo watawala wa ligi hiyo.
Ni ukweli uliowazi kuwa vilabu vya simba na yanga ukichunguza namna
vinavyoendeshwa utagundua kuwa ni kama miradi ya watu binafsi ambao
wanatumia wafuasi lukuki wa timu hizo kujiongezea kipato.Wachezaji wengi
wanaonunuliwa kwa bei kubwa hasa wale wanaotoka nje ya nchi,wanaletwa
kwa pesa za watu binafsi,wanapewa magari,nyumba na mishahara yao kutoka
mifukoni mwa watu wanaoziongoza klabu hizo.
Watanzania wa leo si sawa na wale wa mwaka 47,siku klabu ya Pamba ya
Mwanza au Ujenzi ya Rukwa zitakapopanda daraja na kushiriki ligi
kuu,itakuwa ni sawa na ujio mpya wa Mbeya City. Kutokana na Propaganda za
kila siku ndani ya klabu za Simba na Yanga, watu wamechoka na
wanachosubiri ni kuja kwa timu ambayo wataamini imekuja kuleta
mabadiliko ya kweli kama unavyoona watu wa Mbeya na timu yao. Azam Fc
wanatakiwa kujifunza faida ya mashabiki na kubadilisha mwelekeo wao na
kama wataendelea na tabia yao ya kuamini kuwa pesa ndo kila kitu, kuna
uwezekano watakuja kuzidiwa mashabiki hata na timu ya Lipuli fc kutoka
Iringa.
Kuna timu nyingi tu duniani zinazomilikiwa na watu binafsi kama ilivyo
kwa Azam FC, Chelsea inamilikiwa na Roman Abramovic, Manchester City
inamilikiwa na Sheikh Mansour, AC Millan inamilikiwa na Silvio
Berlusconi na nyingine kibao.Sio Azam FC tu inayotumia watoto wa mmiliki
kuwa sehemu ya bodi ya timu hiyo hata AC Millan pia inamtumia Barbara
Berlusconi binti wa mmiliki wa klabu hiyo kama sehemu ya wakurugenzi
wake lakini, bado mashabiki wamepewa kipaumbele cha juu achilia fedha
walizonazo wamiliki wa klabu hiyo.
Kitu kikubwa kinachowasumbua Azam FC ni kutaka kupambana na klabu za
Simba na Yanga ndani ya jiji la Dar es Salaam na kusahau kuwa,Tanzania
ina mikoa zaidi ya 25 kwa sasa.Azam FC ni wageni kwenye viwanja vyote vya
ligi kuu Tanzania hadi kwenye uwanja wao wenyewe wa Azam Complex pale
Chamazi jiji Dar es Salaam na hili lilijidhihirisha kwenye mchezo wao
dhidi ya Mbeya City kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara
ambapo karibu maelfu ya wakazi wa Mbeya walivamia kiwanja cha Azam
Complex.
Timu ya Mbeya City imejenga tabia ya kutembelea wagonjwa waliolazwa
Hospitalini wakiwa mbeya na nje ya mkoa huu kwenda kuwajulia hali na
kuwapa mkono wa pole.Hii kitu unaweza usiielewe kwa haraka
lakini,inatengeneza mahusiano mazuri sana kati ya timu na wananchi.Azam FC mnaweza kufanya kitu kingine hata kujichanganya na watoto wa shule
mikoani.Hii inaweza kuondoa taswila iliyopo sasa kuwa Azam
haijichanganyi,wamejitosheleza n.k Watanzania wanawahitaji,wapeni nafasi
kwenye timu yenu.
Hata kama wakianza kugawa mikate bure, hii timu haikubariki bara, wataambulia patupu
ReplyDeleteAzam Fc ni timu ya Dar es Salaam kama Simba,Yanga,Ashanti hivyo hailazimishi mtu kutoka bara kama wewe kuishabikia wewe shabikia mbeya city,katavi rangers, au majimaji ya songea
DeleteTuache na timu zetu watoto wa ilala
Unatoka povu bila sababu, hii timu haikubaliki. Pamoja na uwekezaji wote, hata kwa mapato ni ya tano, jiulize. Mo na kajumulo wsnalijua hilo saana.
DeleteKaka umesahau kuwa hizi timu zilikuwa na washabiki hata kabla ya kuja wamiliki!! Leo hii mmiliki wa Azam akiamua kuimiliki yanga au simba washabiki wake hawatahama!! Kwahiyo kuifananisha Azam na akina chelsea ni sawa na kufananisha uji na mtori
ReplyDeleteushauri wako ni mzuri unahitaji muda kwani hata Arab Contractors ya Misri na Safari Sound Contractors ya Tanzania chini ya Hugo Kisima zilijaribu uwekezaji huo zikakosa support ya washabiki kwa dhana kwamba huwezi kununua washabiki.Kwa maoni yangu Azam bado wana nafasi ya kutengeneza mashabiki kwa kuanzia Mbagala ambako Mbagala Market iliweza kuwa na washabiki wengi kabla ya kununuliwa na Mo Dewji.Kinachohitajika ni kujishusha kuwa karibu nao
ReplyDeleteAzam Fc ina mchango mkubwa sana sisi tuliosoma chemistry tunaita catalyst kwenye mpira wetu, sasa hivi kila timu inataka kuwa kama Azam Fc mfano mbeya city wanataka kujenga uwanja,simba wanmehamasika na mapanga kule bunju.
ReplyDeleteKilimanjaro Lager ilibidi iwape mabasi simba, yanga na taifa stars kama la azam fc badala ya coaster
Ni kweli kuna shida katika PR department ya Azam Fc ipo mbali sana na washabiki wake mfano jezi zake ni nzuri sana watu wanataka sana wao wapo kimya. Mbeya city inategemea Jezi kama chanzo cha mapato lakini azam fc wao wala hawajiangaishi na team promo kit
Mchango Wako mzuri. But azam haijaanzishwa 2007. Imeanzishwa chini ya mwaka Huo na ilianza kucheza madaraja ya chino
ReplyDeleteuouo
ReplyDeletePointi zako na ushauri ni kidoogo kuliko mlolongo wa upuuzi ulioandika kujaza kurasa...
ReplyDeleteWatanzania tulio wengi hatupendi kukosolewa..... wengi hawaipendi Azam fc kwa kuwa tu ni tishio kwa vilabu pacha vya Kariakoo. Suala ushabiki ni jambo la mfumo katika uendeshaji wa club. Nini management inataka.... Azam fc ni moja kati ya bidhaa zinazozalishwa na SSB naomba ieleweke hvy hata ikawaje mashabiki hatuwezi kuwa na nguvu kuliko mmiliki. Unataka jersey za Azam fc ziuzwe vp? Azam wanajaribu kulinda brand yao pasipo mtu kujinufaisha kupitia wao. Suala la club kuwa mbali na mashabiki hili usishangae kwa Azam fc coz ni ukweli usuopingika kuwa club ina kila kitu kasoro Fan Base na fan base huwezi kulinganisha Mbeya city ama Coastal na Azam fc. Mbeya inachukuliwa kama club ya wanambeya... Coastal inachukuliwa kama kama ya wanatanga kwa sasa Azam fc maskani ni Chamazi mkoa wa Dar ambapo tayari wenyeji wenyewe wa kariakoo wapo hvy ni vigumu sana. Uahafanya research khs wakazi wa Chamazi na Azam fc? Wengi tunajiridhisha kwa kuamini Azam fc ina wapenzi wa kununua na sio wenye mapenzi ya dhati na club, hili si la kweli sema kinachotuponza watz wengi ni kuona kitu fulani hakiwezi kutokea na ndio maana leo mtu akisema mm Azam fan basi ataambiwa "huna lolote unajiforce tu wewe Simba ama Yanga"
ReplyDelete