Ikumbukwe
kuwa hivi karibuni , uongozi wa Yanga uliitisha mkutano Mkuu wa dharura
uliokuwa ufanyike tarehe 18 Agost 2013 viwanja vya sabasaba
kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 Asubuhi kwa lengo la kujadiliana na suala la Azam
Television kurusha mechi za Yanga. Mkutano huo kwa sasa umeahirishwa kutokana
na sababu ifuatayo
Tarehe
14.8.2014 Naibu Waziri wa Habari, Utamadun,Vijanai na Michezo Mheshimiwa Amosi Makala aliitisha
kikao cha pamoja ,kilichojumuisha pande zote husika wakimwemo wasaidizi wake, shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania(TFF),Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi ya vodacom , uongozi wa Yanga sc na
uongozi wa Azam Media.
Baada ya
kikao hicho yafuatayo ni makubaliano yaliyofikiwa
(a)Klabu ya
Yanga itapata fursa ya kushiriki na kupitia katika utengenezaji wa mkataba wa udhamini wa haki za matangazo na
televisheni wa Azam Media ili
kujiridhisha na vipengele vyote vya mikataba kwamba kwa namna yoyote haviathiri
klabu ya Yanga kufuatia uhusiano uliopo wa Azam Media wanaotarajiwa kupewa haki
hizo na Timu ya Mpira Azam FC moja ya
timu pinzani ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom
(b)Kuwepo na
utayari kwa uongozi wa Azam Media kukutana na uongozi wa Yanga kuzungumzia
mahusiano ya kibiashara yatakayo nufaisha pande zote mbili.
Hivyo basi baada
ya kuzingatia hayo uongozi unapenda kutoa taarifa kwa wanachama wake kuwa
mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 18 Agosti 2013, viwanja vya sabasaba kwenye
ukumbi wa PTA Saa 3:30 asubuhi umeahirishwa hadi mtakapotangaziwa vinginevyo,
lengo ni kutoa nafasi na fursa kwa uongozi kufanyia kazi hayo yaliyotajwa hapo
juu
Pia uongozi
unawashukuru wanachama na wapenzi wote wa Yanga kwa kuonyesha ukomavu na
kusimamia maendeleo ya klabu yetu kwa
Hali na mali, na uongozi Utaendelea kusimama IMARA katika kuijenga Yanga Mpya
Uongozi pia
unawataka wapenzi wote kuja kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yetu wakati wa
mechi ya kugombea ngao ya hisani kuashiria ufunguzi wa michuano ya kutetea
ubingwa tunaoushikiria wa Ligi Kuu ya
vodacom
Clement
Sanga
Makamu Mwenyekiti
Young
Africans Sports Club
16.08.2013
No comments:
Post a Comment