MATCH REPORT: SIMBA VS VITAL'O - FIRST HALF
Vital'O waliuanza mchezo vizuri, wakitawala vilivyo mchezo ndani ya kipindi chote cha kwanza na wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini kukosa umakini na umahiri Juma Kaseja walizipoteza nafasi hizo.Kwa upande wa Simba wakiwa wamewaanzisha wachezaji wao wapya mabeki Derrick Walulya na Saidi Nassoro Cholo, Ulimboka Mwakingwe, Haruna Moshi na Salum Machaku walionekana kukosa maelewano na hivyo kupelekea kushindwa kucheza vizuri ndani kipindi hiki ingawa wachezaji kama Ulimboka Mwakingwe, Boban na beki Said Nassoro Cholo walionekana kucheza vizuri.
Ndani ya kipindi kwanza Simba walicheza faulo 14, Mgosi akicheza 5, Boban 3, Cholo 1,Maftaa 3, Santo akacheza 2 na kupata kadi moja ya njano.
Vital'O walicheza faulo 8.
Kona- Simba 5, Vital'O - 1
SECOND HALF
Kipindi cha pili Simba waliuanza mchezo kwa kasi Boban,Machaku na Mwakingwe wakilisakama lango la Vital'O, lakini kutokana na kukosa umakini kwa mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi aliyecheza chini kiwango Msimbazi walishindwa kupata bao.
Vital'O ndani second half walionekana kuchoka na kutokana Simba kuwashambulia sana walianza kucheza rafu zisizo na msingi hasa kwa Boban.
Waburundi hawa baada ya kipindi cha pili kuanza walifanya mabadiliko kwa kumtoa Stanley Minzi na kuingia Mbakiye Beby Miami, pia walimtoa Ndizeye Alain akaingia Garukwishika Jean.
Simba waliwatoa Salum Machaku, Banka, Mgosi na nafasi zao zilichukuliwa na Shija Mkina, Patrick Mafisango na Rajab Isiaka.
Kipindi cha pili Simba walicheza Faulo 4, huku Vital O wakicheza faulo 10 na kupata kadi 1 ya njano.
MAONI YA MAKOCHA
Mosses Bassena-"Timu yangu ilijitahidi kucheza vizuri na kumiliki mchezo kwa zaidi ya asilimia 70, na tumepoteza nafasi nyingi za kufunga hasa ndani ya kipindi cha pili lakini haikuwa siku yetu hasa kwa Mgosi ambaye leo hakuwa ndani ya kiwango chake.Tunajipanga kucheza vizuri katika michezo inayofuatia ili tuweze kufanikisha adhma yetu kubeba kombe hili."
YAOUNDE KANYANKOLE - VITAL'O COACH
"Nashukuru timu imepata sare dhidi ya timu kubwa kama Simba tena ukizingatia tulikuwa tunacheza mbele ya maelfu ya washabiki wa wapinzani wetu lakini vijana wangu wamejitahidi na tumefanikiwa kupata sare.Naamini tutajipanga na kupata ushindi katika mechi zijazo.Simba ni timu nzuri japo wanaonekana hawajazoeana lakini naamini wakikaa muda mrefu watakuwa na timu bora."
Shafii your selfish, mbona mechi ya yanga hadi vikosi umeweka ila simba umebana kiasi hicho....!! kumbuka wewe ni mwana habari na c mwana yanga
ReplyDelete