Search This Blog

Friday, June 24, 2011

USAJILI WAZIDI KUPAMBA MOTO BARANI ULAYA.


Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa paundi million 26.5 kwa ajili ya mshambuliaji wa F.C Porto Radamel Falcao, baada ya mkorombia huyo kukubali deal la kuvuna paundi million 5 kwa mwaka na matajiri hao London.

Falcao ambaye alifunga mabao 39 katika msimu uliopita anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea tarehe 1 Julai.

Usajili huu wa Falcao umezua maswali mengi kuwa ni nani kati ya Fernando Torres, Didier Drogba na Nicolas Anelka atafunguliwa milango ya kuondoka Stamford Brdige.


ARSENAL WAKATAA OFA YA PAUNDI MILLION 27 KWA FABREGAS


Klabu ya Arsenal imekataa ofa paundi million 27 kutoka Barcelona kwa ajili ya kiungo Cesc Fabregas.

Barca ambao wamekuwa katika harakati za kumrudisha Catulunya kwa zaidi ya miaka 3 lakini Gunners siku zote wamekuwa wagumu kumuachia Mhospania huyo.

Ripoti zinasema kuwa CEO wa Arsenal Ivan Gazidis aliikataa ofa rasmi ya Barca iliyowasilishwa na makamu wa raisi wa mabingwa hao Ulaya Maria Bartomeu ambaye alikuwa London wiki iliyopita.Hata hivyo taarifa kutoka vyanzo vya habari kutoka Nou Camp zinasema Barca wanajipanga kupeleka tena ofa nyingine kwa Arsenal ndani siku chache zijazo.


Wakati huo huo manager wa klabu ya Barcelona Pop Guardiola amesema kuwa usajili wa Fabregas kipaumbele cha kwanza katika mipango ya kukimarisha kikosi chake.

Akiongea na vyombo vya habari vya Spain Gurdiola alisema: "Kumsajili Cesc ndio kipaumbele cha kwanza katika usajili wa msimu huu kwa sababu ndiye mchezaji ambaye yupo katika mipango ya muda mrefu ya klabu hii."


MAN CITY WAMGEUKIA MATA


Baada ya kutoswa na Alexis Sanchez sasa matajiri wa EPL Manchester City wanajipanga kumsajili winga wa Valencia ya Hispania Juan Mata.

Mabingwa hao FA Cup wanajipanga kukiongezea ubora kikosi cha Roberto Mancin ambacho kimepata nafasi ya kushiriki katika ligi wa mabingwa wa ulaya msimu ujao.

City ambao juzi ripoti kutoka Chile zinasema baada ya klabu hiyo kuizidi mbio Barca za kumsajili Sanchez, walipewa nafasi ya kuongea na mchezaji mwenyewe lakini Sanchez aligoma kuongea na timu hiyo, lakini katika hali nyingine jana mmiliki wa Udinese Gianpaolo Pozzo alisema mchezaji huyo anauzwa kwa paundi million 44, kiasi ambacho kimeongeza ugumu katika suala la mchile huyo hivyo kuwafanya City kumgeukia Juan Mata kama mbadala.

Juan Mata kwa sasa yupo katika kikosi Spain under 21 katika michuano ya EURO under 21.


LIVERPOOL KUTOA OFA YA PAUNDI MILLIONI 10 KWA CHARLIE ADAM



Majogoo wa jiji Liverpool wanategemea kuwasilisha rasmi ofa paundi million 10 kwa ajili ya kupata huduma za kiungo Charlie Adam katika mazungumzo yao na klabu ya Blackpool yaliyopangwa kufanyika weekend hii.

Kiungo mwenye umri wa miaka 25 pia amekuwa katika rada za Sir Alex Ferguson lakini Liverpool wanaonekana kuwa nafasi zaidi ya kupata saini ya kiungo huyo ambaye walitoa ofa ya paundi million 8 mwezi January lakini Blackpool wakachomoa.

Liverpool wanatarajiwa kukutana na mwenyekiti wa Blakcpool Karl Oyston.


No comments:

Post a Comment