Meneja wa kinywaji cha GUINNESS, Maurice Njowoka akitoa ufafanuzi wa namna ya shindano la Guinness Football Challenge litakavyofanyika mapema leo mbele ya wanahabari,kwenye ofisi za makao makuu ya kampuni ya bia ya Serengeti,Oysterbay,jijini Dar.
Mashindano ya Guinness Football Challenge yanatarajiwa kufanyika hapo kesho kwenye viwanja vya Leaders,Kinondoni. kwa mujibu wa Meneja wa kinywaji cha Guinness bwana Maurice Njowopa,shindano hilo litashirikisha watanzania wote wenye jinsia zote kuanzia umri wa miaka 18. shindano hilo litagawanyika katika sehemu kuu mbili
i) uwezo wa kuuchezea mpira
ii ) uwezo wa kujibu maswali
kutokana na mgawanyo huo hapo juu kila timu inatakiwa kuwa na watu wawili mmoja katika kila kipengele, na timu nane zitakazokusanya pointi nyingi zitapata nafsi ya kwenda nchini afrika ya kusini kushindania kiasi cha dolla za kimarekani 50,000 zitakazotolewa kwa mshindi wa kila wiki katika shindano hilo litakalochukua majuma manane.
Pichani kulia ni muwakilishi wa kampuni ya Endemol ya nchini Afrika Kusini,Warren na mwisho kushoto ni Muwakilishi wa kampuni ya Carberry Commonication,Tom akiwa pamoja na Meneja masoko wa kinywaji cha GUINNESSS,Moses Kebba walipokuwa wakizungunza na Wanahabari jijini Dar leo.
No comments:
Post a Comment