Search This Blog
Tuesday, August 30, 2011
Barcelona 5-0 Villarreal: Guardiola abadili mfumo dhidi ya Villareal.
MFUMO WA BARCELONA KIUNDANI.
Barcelona waliifunga Villareal bila hururma kwa mabao 5-1 na kuwajibu wapinzani wao Madrid ambao waliwafunga Zaragoza mabao 6-0.
Pep Guardiola aliwakosa Dani Alves , Carles Puyol na Gerard Pique hivyo akamchezesha Eric Abidal na akawatumia Sergio Busquets na Javier Mascherano kwenye ulinzi.
Xavi Hernandez na David Villa waliwekwa benchi huku Thiago Alcantara, Cesc Fabregas na Alexis Sanchez wote wakianza .
Juan Carlos Garido alipanga timu ile ile ya Villareal iliyotegemewa na wengi ambapo Bruno Soriano alirudi kwenye sehemu yake ya kiungo baada ya kuwa amecheza kaka beki katikati ya wiki na Gonzalo Rodriguez alirudi kucheza beki.
Mchezo huu ulikuwa si wa ushindani kama ule uliozikutanisha timu hizi mwaka jana . Villareal walikuwa hawana mashambulizi kabisa na walifia mikononi mwa Barca kwa urahisi ambao hakuna aliyeutegemea.
MFUMO WA BARCA UKIWA UMETENGWA.
Kwanza, kulikuwa na mfumo usioeleweka uliotumiwa na Barcelona na ulionekana kufanya kazi uwanjani kwa kiwango kikubwa sana .
Mfumo huu ni wa 3-4-3 huku wachezaji wanne wa katikatiya uwanja wakicheza kwa mfumo wa ‘diamond’, ni wachezaji wawili tu ndio waliobaki kwenye sehemu zao muda wote nao walikuwa beki wa mwisho Sergio Busquets na kiungo mkabaji Seydou keita.
Eric Abidal na Javier Mascherano walikuwa wanaingia ndani kidogo wakati mwingine huku wakijaribu kuwarudisha nyuma Giuseppe Rossi na Nilmar. Viungo waliocheza nje Andres Iniseta na Thiago Alcantara walijaribu kucheza ndani wakati mwingine wakijaribu kubadilishana nafasi na Cesc Fabregas.
Kwa viungo wepesi kama hao na mkabaji mmoja ambaye ni Seydou Keita mfumo ulionekana kama 3-1-3-3 kwa muda mrefu wa mchezo.
Huku Barcelona wakiwa hawana kabisa mabeki wa pembeni au mawinga, wachezaji watatu wa mbele walizunguka zaidi na kuelekeza mipira pembeni mwa uwanja huku Sanchez na Pedro wakibaki sana pembeni kuliko kuingia ndani ghafla au bila kushtukiza. Kwa yote Mfumo huu ulionekana kuendana kidogo na mifumo ya kocha wa zamani wa Chile Marcelo Bielsa
Mfumo sahihi wa kucheza dhidi ya Villareal.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Barcelona kwa msimu huuna kuna imani kubwa kuwa hii inaweza kuwa timu yao ya kwanza kwa msimu huu. Kuna tahadhari ya ziada inahitajika hapakwa kuwa Guardiola ana historia ya kucheza kwa kutuma mifumo isiyo kawaida kwa timu yake kwenye baadhi ya mechi ili kukabili kitu husika toka wapinznai wake.
Alichezesha mfumo wa 3-4-3 kwenye mchezo dhidi ya Atletico Madrid msimu uliopita kwa lengo la kuwasukuma mawinga wa timu pinzani kwenye eneo lao , pia aliwahi kumtumia Dani Alvez kama winga kwenye mechi dhihi ya Sevilla . Mara nyingi pia huwa anajaribu kitu tofauti kwenye michezo dhidi ya timu zenye washambuliaji wawili .
Mfumo huu hivyo ulikuwa sahihi kwa Villareal. Kwa kawaida wanachezesha mfumo wa 4-2-2-2 huku kukiwa na viungo wawili wanaocheza pembeni na wakati mwingine wanaingia ndani , na mara nyingine wanacheza 4-3-1-2, vyovyote ni mfumo ambao unabana uwanja .
Kwa kuanzia nyuma , Barca walikuwa na mtu wa ziada . Mascherano alikuwa anamkaba Rossi na Abidal alimkaba Nilmar kwani washambuliaji hao huwa wanacheza kila mmoja akienda upande wake pembeni mwa uwanja huku Busquets akiwa kama mtu wa mwisho asiye na jukumu maalum.
Hatari moja ya kucheza dhidi ya mfumo wa Villareal wa 4-2-2-2 ni kwamba wakati mwingine wanakuwa na viungo wa kati wanne ila kwa kuchezesha mfumo wa ‘diamond’ , Guardiola alikuwa anawakabili kwa kuhakikisha muda wote inakuwa vita ya 4v4 . Mbele zaidi mabeki wa pembeni wa Villareal ambao kwa kawaida huwa wanapanda kupunguza uwanja walibanwa na Pedro na Alexis Sanchez na hakuna mfumo bora zaidi ya huu wa kuutumia dhidi ya Villareal.
Timu zilivyoanza .
Ulikuwa mchezo wenye vita ya mifumo ndani yake.Kwa Barcelona mfumo wao ulikuwa na chembechembe nyingi za kufanana na ule wa Liverpool wakati Kenny Dalglish alipoiongoza timu yake kuifunga Chelsea mapema mwaka huu.
Carlo Ancelotti akiwa ndo kwanza amesajili Ferando Torres alichezesha mfumo wa 4-3-1-2 huku akiweka mtu wa ziada nyuma kusaidia ulinzi, Dalglish aliamua kuwapanga mabeki wa kati watatu huku akipanga viungo wanne ambao wanacheza kwenye shape ya’diamond’.
Tofauti ilikuwa mfumo wa Dalglish ulikuwa wa kasi zaidi ya ule wa Barca nah ii ni kwa sababu Liverpool kiasili hupendelea soka la mwendo wa kasi kama ilivyo kwaingereza wengi , Dalglish pia alitumia mawinga ambao ni mabeki na walifanya kazi ile ile ya mabeki wa pembeni.
Jinsi Barca walivyoshinda.
Bao la kwanza lilionekana kuwa la kiufundi haswa kwa kuwa lilikkuja toka kwa mchezaji wa Barcelona mwenye uhuru wa kufanya atakacho uwanjani.
Mfumo wa Villareal ulikuwa unatumia viungo wawili wakabaji, wakiwatumia Valero kama mharibifu wa mashambulizi ya wapinzani na mwenzie Cani akiwa mbali naye kkidogo pembeni uliwafanya Barca wamiliki mpira kirahisi.
Hili lilionekana kufanya kazi kwa kiasi Fulani mwanzoni pake ambapo Cani alionekana kama anaipenya ngome ya Barca, anaweza kuona kama anafanya jamba la msingi lakini katika hilo alikuwa anampa mwanya Thiago Alcantarra .
Hiyo ndio sababu kuu ya kwanini Alcantarra alipewa uhuru aliopewa katikati mwa uwanja, na madhara yake ni pale alipofunga bao rahisi ambapoa li-drible toka mbali hadi nje ya 18
Bao la pili lilionyesha mchango wa Cesc Fabregas kwenye timu hii.
Kitu ambacho wengi wanaweza kubisha ni ukweli kuwa Fabregas alikuwa anahitajika kwenye timu hii na ndio maana amekuja , msimu uliopita Barca walikosa mchezaji kama huyu. Alichokuwa anafanya Cesc ni kukimbia toka eneo la katikati mwa uwanja huku akifaidika na Movement za Lionel Messi.
Wakati mwingine Iniesta alionekana kufanya kazi hii japo anapenda kuingia ndani sana . Fabregas ni mtu sahihi wa kuiongezea Barcelona ‘movement’ za ziada katika ya uwanja-sio namba 10 wa asili lakini ni mchezaji anayependa kupandisha timu akiwapa presha mabeki . Uhusiano wake uwanjani na Messi unaonekana kufanya kazi vyema hadi sasa na ni rahisi kuona hivyo kwa kuwa amekuwa akifanya hivyo tangu akiwa Arsenal na Van Persie.
Fabregas anaweza kucheza kama ‘namba 9 wa uongo’ na wengine wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa huenda akawa ‘namba 10 wauongo pia’.
Mabao matatu ya Barca ya kipindi cha pili yalikuja kwa kuwa Villareal waliweka mstari wa ulinzi eneo la juu sana na kwa hivyo wakajikuta wakinaswa kwa mtego wao wenyewe.
Mwisho
‘Perfomance’ nzuri toka kwa mabingwa watetezi wa ligi ya Hispania , ufundi hasa kwa Barcelona ulkikuwa wa hali ya juu. Angeweza kuwachezesha wachezaji wanne kwenye eneo la ulinzi labda angemrudisha Keita nyuma kidogo na kumuingiza kiungo kinda Anderu Fontas ila uamuzi wake wa kutumia 3-4-3 ulimlipa na ukawapa ushindi mzuri dhidi ya timu iliyowapa tabu msimu uliopita.
Je utakuwa mfumo mkuu wa Barcelona msimu huu? Labda . Ni muhimu kukumbuka kuwa walicheza na timu inayotumia mfumo huo huo Villareal.
Inaonekana kuwa kama Bracelona watatumia mfumo huu watajaribu kuchanganya na 4-3-3. Kama Pique na Puyol wakirudi kwenye ulinzi na kuwaruhusu Mascherano na Busquets kusogea juu kidogo , wanaweza kutumia mchanganyiko wa mifumo ya 3-4-3 au 4-3-3 huku wakiwa na bei wa kati anayecheza kwa kupandisha timu. Huu ni mfumo unaoweza kuzimudud timu zinazotumia ‘namba tisa’ wa uongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment