Usiku wa jana ulikuwa mrefu sana kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya timu yao kupigiwa soka la hatari na kufungwa 2-0 na mabingwa watetezi wa klabu bingwa ya ulaya FC Bayern Munchen.
Usiku wa jana tulishuhudia Bayern Munich wakiweka rekodi mpya ya Champions League baada ya kukamilisha asilimia 95% ya pasi walizopiga.
Tuangalie ushindi huo wa Bayern kupitia mfumo wa namba.
863
Hii ni namba ya pasi walizojaribu kupiga Bayern, 95% ya pasi hizi zilifika kwa wenzao. Hii ni rekodi mpya katika champions league tangu utaratibu wa takwimu kwenye mechi uanze msimu wa 2003-04 season..
222
Namba ya pasi walizojaribu kupiga Arsenal. Walikamilisha 71% ya pasi hizo. Namba ya chini kabisa kwa Arsenal katika takwimu za pasi, kabla ya jana namba ya chini kabisa ilikuwa 394, hii ilikuwa kwenye EPL dhidi ya Tottenham mwezi September mwaka jana.
147
Hii namba ya pasi alizopiga kiungo wa Bayern Toni Kroos.
127
Namba ya pasi alizopiga Toni Kroos katika nusu ya uwanja golini mwa Arsenal - alikamilisha 96.1% ya pasi hizo.
100
Goli la Toni Kroos jana usiku lilikuwa goli la 100 kwa Bayern Munich katika mashindano yote msimu huu. Kadi nyekundu ya golikipa Wojciech Szczesny ilimfanya kuwa mchezaji wa 100 kupewa kadi nyekundu tangu Wenger aanze kuifundisha timu hiyo mwaka 1995.
78.8
Asilimia ya umiliki wa mpira waliyokuwa nayo Bayern Munich ndani ya dakika 90.
30
Mchezaji aliyejaribu kupiga pasi nyingi zaidi kwa upande wa Arsenal alikuwa Jack Wilshare ambaye alikamilisha 66% ya majaribio 30.
26
Majaribio ya kufunga yaliyofanywa na Bayern katika goli la Arsenal, Arsenal walijaribu mara 8 tu - mara 1 tu katika kipindi cha kwanza.
12
Arsenal waliweza kuwa na jumla ya 12% ya kumiliki mpira katika kipindi cha pili.
3
Winga wa Bayern Munich Arjen Robben ndio mchezaji pekee kuwahi kupewa penati 3 katika msimu huu wa Champions league. Mesut Ozil ndio mchezaji pekee aliyekosa mara mbili.
No comments:
Post a Comment