Nashukuru mwenyezi mungu nimefika salama hapa Ujerumani - tayari kwa ajili ya kuangalia na kukuletea baadhi ya matukio kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kati ya Chelsea na Bayern Munich.
Tangu nifike hapa nimegundua baadhi ya vitu vifuatavyo:
Ticketi ya kiwango cha chini sasa zinauzwa euro 1,500 ambayo ni karibia
milioni 3 ya kitanzania.
Hii inakuonyesha namna gani tukio hili la mchezo
wa fainali ya UEFA Champions League lilivyo kubwa sana.
Makampuni
yanayofanya kazi na UEFA yanafanya sana biashara mfano bia zinazonyweka
hapa ni Heineken tu huku bei ikiwa imeongeka kwa asilimia 100'mwanzoni
glass ya bia ya heineken iliuzwa kwa euro 2.5 lakini sasa imepanda mpaka
euro 5, jezi za Bayern ndio zinanunuliwa sana huku kila jezi ikiuzwa
kuanzia euro 80, ambayo ni kama laki moja na sitini kwa pesa ya
kitanzania, kwakifupi mzunguko wa biashara umeongezeka kwa takribani
juma zima lililopita...
wandugu mnapesa za kuchezea,dunia siku hizi ni kijiji sasa nyie kusema kuwa mnaturetea habari za mpambano wa fainali tunakuwa hatuwaelewi sababu kila mtanzania ana access ya kuangalia mpira kupitia TV iwe bar au nyumbani iweje nyie mseme kuwa mnatuletea mpambano wa fainali.Hii siyo mwaka 47 bwana TV ipo ikulu tu.Mmepoteza pesa zenu tu.
ReplyDeleteShafii hii pesa ya kiingilio siyo kweli hakuna kiingilio cha namna hiyo!!! kwani fainal ya Wembley ilikuwa laki 4,so gape hilo sikubaliani nalo!!!
ReplyDeleteNimeamini soka inalipa.
ReplyDeleteClub zetu za bongo zijifunze kutoka kwa hawa wakubwa.