JEZI
namba 30, aliyokuwa anavaa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika klabu ya Simba, Patrick Mutesa
Mafisango kuanzi sasa haitakuwa ikitumika tena kwa heshima ya mchezaji huyo
aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia jana, jijini Dar es Salaam.
Hayo
yalisemwa jana Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage alipokuwa akihutubia
mamia ya wadau wa soka waliohudhuria zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Mafisango
kwenye viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam, kabla ya kupelekwa Uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, tayari kwa safari ya kwenda kwao,
DRC kwa ajili ya mazishi kesho.
Heshima
kama hiyo alipewa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Marc Vivien Foe na
klabu yake, Manchester City ya England alipofariki Dunia Juni mwaka 2003,
ambapo jezi namba 23 ilitunzwa moja kwa moja.
Aidha
Rage alisema msiba huu ni mkubwa kwa Simba kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa ni
muhimili mkubwa kwa timu hiyo akiwashauri wachezaji na kuwa nao karibu ndani na
nje ya uwanja.
“Mafisango
alikuwa na mchango mkubwa kwa Simba na mara ya mwisho klabu kukumbumbwa na
msiba mzito namna hii ilikuwa ni mwaka 1978 ambapo Simba ilimpoteza mchezaji
wake mahiri Hussein Tidwa na ukweli ni kwamba wachezaji hawa tutawaenzi miaka
yote na ndio sababu ya kutotumia tena jezi namba 30 kwa kuvaliwa na mchezaji
yoyote,” alisema Rage.
Rage
alisema licha ya umahiri wa Mafisango Dimbani pia alikuwa mchezaji ambaye
alitoa mchango mkubwa na hasa wachezaji wawapo nje ya nchi kutokana na umahiri
wake wa kujua lugha mbalimbali ambapo alikuwa akiwasaidia wachezaji wenzake.
“Ni
pengo kubwa kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa akijua lugha nyingi ikiwemo
Kiswahili, Kingereza na Kifaransa na
kuwasaidia wachezaji walipokuwa nje ya nchi tutamkubuka sana Mafisango,” aliongeza.
Kutokana
na machungu ya msiba huo Rage alishindwa kumaliza kusoma risala fupi ya
marehemu mara baada ya kuishiwa nguvu na kumwaga machozi na kupelekea Makamu
Mwenyekiti wa klabu hiyo Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kumsaidia kusoma risala hiyo.
“Mfisango
ni mchezaji ambaye alikuwa akijituma nje na ndani ya uwanja na kabla ya kutua
Simba Marehemu aliwahi kucheza soka katika timu mbalimbali ikiwemo Tp Mazembe
ya DRC, APR ya Rwanda , Azam na Simba za Tanzania na pia alikuwa Nahodha wa
timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ alisema Kaburu.
Wakati
wa kutoa heshima za mwisho katika uwanja wa Sigara maelfu ya watu walijitokeza
uwanjani hapo wakiongozwa na mchungaji Tito Kihame ambaye aliongoza ibada ya
kuuga mwili wa marehemu, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella
Mukangara na viongozi mbalimbali wa serikali na viongozi kutoka klabu mbalimbali
za hapa nchini.
Mukangara
aliwataka wachezaji wa Tanzania kujituma na kuwa na moyo kama ambao alikuwa nao
Marehemu Mafisango kwa kujituma na kuwa na jitihada za zaidi nje na ndani ya
uwanja kama ambavyo marehemu alivyokuwa akifanya.
“Kifo
chake ni pigo kubwa kwa Simba na Watanzania kwa ujumla na tunamshukuru kwa
kuvuka mipaka na kuona umuhimu wa kuja na kucheza Tanzania na pia wachezaji wa
Simba wasikate tamaa cha muhimu waendeleze kile ambacho alikiacha marehemu,” alisema
Mukangara.
“Ukweli
ni kwamba katika familia ya soka hapa nchini tumepoteza mtu muhimu sana na
tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani,” alisema Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Soka Tanzania TFF Angetile Osiah.
“Sisi
Simba ni watani zetu na tunakuwa pamoja katika shida na hivyo basi mimi kama
kiongozi wa Yanga nimeiwakilisha klabu nzima na tutaendelea kuwa bega kwa bega na
watani zetu katika kipindi hiki kigumu ila mchezaji Mafisango alikuwa ni
mchezaji hodari uwanjani hivyo basi anastaili kuigwa na wachezaji wengine,” alisema
Selestine Mwesigwa katibu Mkuu wa Yanga.
Nao
wachezaji mbalimbali kutoka timu ya Taifa Taifa Stars walijitokeza na kubeba
jeneza la mchezaji mwenzao na kuliingiza katika viwanja vya Sigara wachezaji
hao Juma Kaseja, Jonh Bocco, Mwinyi Kazimoto, Shabani Nditi, Amiry Maftah,
Nurdin Bakari, Agrey Moris na Juma Nyoso.
Profesa Philemon Sarungi akimsaidia Rage |
Mara
baada ya nyota hao kuufikisha mwili wa marehemu katika sehemu husika ambayo
ilipangwa Kazimoto na Kaseja iliwalazimu watu wa ziada kujitokeza na kuwapa
sapoti mara baada ya kushindwa kutembea na kuwapeleka katika eneo husika ambalo
walikuwa wamepangiwa kukaa.
Katika
hatua nyingine Ofisa habari wa wekundu hao wa Msimbazi Ezekiel Kamwaga ‘Mr
Liverpool’ alisema kuwa katika msafara wa leo kuondoka kwenda Kongo kuusafirisha
mwili wa marehemu kwa niaba ya wachezaji atawawakilisha Haruna Moshi ‘Boban’
ambaye alikuwa karibu na marehemu pamoja na mjumbe wa kamati ya utendaji ya
klabu hiyo Joseph Itang’are.
“Mwili
wa marehemu utaondoka mapema alfajili ya kesho (leo) kwenda kwao Kongo ila pia
leo mtoto wa marehemu Chris Paul,
mwenye umri wa miaka mitano ameondoka na mchezaji wa Yanga Haruna
Niyonzima ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda,” alisema Kamwaga.Picha na habari kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/
Oh my goodness! Incredible article dude! Thanks, However I am going through issues with
ReplyDeleteyour RSS. I don't know the reason why I cannot subscribe to it.
Is there anybody getting similar RSS problems? Anybody who knows the answer can
you kindly respond? Thanks!!|
Look into my web blog :: pit 37 pdf [contentoanimation.com]