Papa wa kanisa katoliki duniani amealikwa rasmi na klabu ya FC Barcelona kupitia Raisi wa timu hiyo Sandro Rosell kwenda kutembelea na kuangalia mechi kwenye dimba la Nou Camp.
Mkuu huyo wa kanisa katoliki, Papa Francis, ni shabiki wa klabu ya nyumbani kwao San Lorenzo na amekuwa akizivutia timu nyingi tangu alipochaguliwa kuwa Papa mwezi uliopita.
Mastaa wa Argentina kama mshindi wa mara nne wa Ballon d’Or Lionel Messi na mchezaji wa zamani wa Liverpool Javier Mascherano kwa sasa wapo kwenye kikosi cha Blaugrana, na Rosell anasema litakuwa jambo la maana ikiwa mkuu huyo wa Wakatoliki kuweza kuhudhuria mechi mojawapo ya Barca.
Alisema kwenye barua iliyochapishwa na gazeti la El Mundo Deportivo: "Kama Raisi wa Barcelona na itakuwa jambo la heshima kubwa kushea na wewe kitu ambacho wote tunakipenda nacho ni mchezo wa soka.
"Ningependa kukaribisha kuangalia mechi kwenye dimba la uwanja wa Camp
Nou na kufurahia mchezo wa soka kutoka kwa wachezaji wetu, hasa waargentina wenzio Messi na
Mascherano, ambao wamesapoti mualiko huu kwa kuweka saini zao kwenye barua hii.”
No comments:
Post a Comment