Na Baraka Mpenja Dar
es Salaam
Mlinzi wa kushoto wa klabu ya
maafande wa jeshi la kujenga taifa wa JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani, Stanley
Nkomola, amesema ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu ni ngumu sana kwao na
wanahitaji kupigana kufa na kupona ili kukwepa panga la kushuka daraja.
Akizungumza katika mahojiano maalumu
na mtandao huu, Nkomola amesema timu ikiwa na pointi 31 kwenda juu inaweza
kujinusuru na mkasi wa kushuka daraja, lakini chini ya pointi hizo inaweza
kuporomoka daraja.
“kwa sasa tuna pointi 22 na aprili 10
tunakutana na wagosi wa kaya Coastal union uwanja wa mkwakwani Tanga,
tunahitaji ushindi ili angalau tufikishe pointi 25 na kuendeleza harakati za
kubakia ligi kuu msimu ujao”. Alisema Nkomola.
Mchezaji huyo aliongeza kuwa kila
mchezaji sasa ametambua kuwa anatakiwa kuwajibika kwa nafasi yake, kwani klabu
hiyo ikishuka daraja itakuwa balaa mkoani Pwani na jeshi kwa ujumla.
Pia Nkomola alisisitiza kuwa kubwaga
manyanja kwa kocha wao mkuu Charles Kilinda kumewaathiri sana kiuchezaji kwani
wamekosa mambo mengi ya kiufundi kutoka kwa kocha huyo.
“Unajua kuondoka kwa Kilinda ni sawa
na kuondoka kwa mzazi, lakini tumejipanga ipasavyo kuibakisha timu ligi kuu na
yeye atakaposikia atafurahi sana”. Aliongeza Nkomola.
Akiongelea suala la mashabiki wa
klabu hiyo kukosa imani na timu hiyo, mchezaji huyo alisema klabu hiyo haiwezi kushuka
daraja kutokana na mipango yao ya sasa.
Maafande wa JKT Ruvu wapo nafasi ya
10 katika msimamo wa ligi kuu, nyuma yao kuna timu za Tanzania Prisons wenye pointi 20 nafasi ya
kumi na moja, nafasi ya 12 wapo Africa Lyon wenye pointi 19, nafasi ya 12 wapo
maafande wa Polisi morogoro wakiwa na poniti 18 na mkia unashikiliwa na Toto
Africans wenye pointi 18.
No comments:
Post a Comment