Na Baraka Mpenja Dar
es Salaam
Wawakilshi pekee wa Tanzania michuano
ya kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya Azam fc maarufu kama wana
lambalamba wanaendelea kupanga majeshi ya kuwashambulia wapinzani wao Barrack
YC ya Liberia mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho utakaopigwa kesho
kutwa dimba maridhawa la Taifa jijini Dar es Samaam.
Afisa habari wa klabu hiyo ,Jafar Idd
Maganga, amesema wanaendelea na maandalizi huku wachezaji wote wakiwa barabara
kuwakabili wapinzani wao.
Idd alisema kuwa mshambuliaji wao nyota
kutoka nchini Uganda, Brayn Umony, umejiunga na wenzake baada ya kukaa nje ya
uwanja akisumbuliwa na majeraha.
“Jioni ya leo tumefanya mazoezi
uwanja wa taifa ili kuuzoe kabla ya mchezo wetu wa jumamosi, hapo kesho
tutafanya mazoezi ya mwisho Chamazi kama sehemu ya kuwapisha ndugu zetu kutoka
Liberia kufanya mazoezi yao ya mwisho uwanja wa taifa”. Alisema Idd.
Pia aliongeza kuwa hapo jana na leo
wapinzani wao wamefanya mazoezi katika uwanja wa Chamazi na kufurahia mandhari
ya uwanja huo.
“Barrack Yc hawajaamini kama sisi
tunamiliki uwanja bora kama ule, wametupongeza sana na kukutakia kila la heri”.
Alisema Idd.
Afisa habari huyo aliwataka
watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa taifa siku ya jumamosi ili kuwaunga
mkono kama walivyofanya mechi za nyuma.
Alisema katika michezo ya kimataifa,
kinachotakiwa kwa kila mdau wa soka ni kuvaa uzalendo na kuishangilia timu ya
nyumbani bila kujali unazi wa timu.
“Timu imeaandaliwa muda mrefu,
kilichobaki ni kuwapanga wachezaji kisaikolojia kwa ajili ya mechi hiyo,
Watanzania waje kutuunga mkono kwani tutawapa zawadi ya ushindi mnono nyumbani
kwetu”. Alisisitiza Idd.
Azam fc imefikia hatua hiyo baada ya
kuwatungua wasudani kusini, Al Nasri Juba mabao 3-0 uwanja wa taifa na mechi ya
marudiano ugenini, wakaishushia dhahama ya mabao 5-0 na kusonga hatua
inayofuata kwa wastani wa mabao 8-1.
Ilipoenda nchini Liberia klabu hiyo iliwafunga
wapinzania wao Barrack YC mabao 2-1 na sasa inahitaji sare yoyote au ushindi
kuwatupa nje waliberia hao.
Barrack Yc wanahitaji ushindi wa
mabao mawili kwa nunge ili waitoe klabu ya Azam Fc.
Mungu ibarike Azam fc, mungu ibariki
Tanzania.
No comments:
Post a Comment