Search This Blog

Friday, April 5, 2013

DEMBA BA: HAYA NDIO MAANDALIZI YANGU YA SIKU NZIMA KABLA YA MECHI KUBWA


Alfajiri

“Nikiwa kama muislamu najaribu kuwa nasali mara tano kwa siku. Sala ya alfajiri huwa ndio ya kwanza - hivyo mara nyingi naamka mpaema na kusali, kusali ni moja ya sehemu kubwa ya maisha yangu

Saa 4 Asubuhi

“Siku zote huwa nalala kabla ya 11.30pm, lakini silali sana. Ikiwa tunacheza mechi 3pm siku ya Saturday kawaida naamka mida ya saa 4-5 asubuhi.

Saa 4.30 asubuhi

“Pindi niamkapo napendelea kula mayai. Mayai ni mazuri na pia kuna chakula fulani cha kisenegal kinaitwa thiakry. Ni mchanganyiko wa yoghurt na aina fulani ya ngano, pamoja na sukari ndani yake.

Saa 5 asubuhi

“Ikiwa tunacheza nyumbani napendelea kukaa nyumbani na familia yangu na kupumzika. Ni jambo zuri kuwa nao karibu kwa sababu wanaiondoa akili kwenye kuifikiria mechi.”

Saa 5.30 asubuhi

“Napendelea kuruka kamba asubuhi. Ni zoezi zuri kwa moyo wangu, linatengeneza vizuri mapigo yangu ya moyo hali ambayo inaniandaa vizuri kwa mchezo.

Saa 7 mchana

“Huwa naenda uwanjani masaa mawili kabla ya mchezo. Pindi ninapofika uwanjani naanza kuweka akili yangu kwenye mchezo, wakati huo huo nakuwa nimeweka headphones kwenye masikio yangu na kusikiliza Quran –kitu hichi kinakuwa kizuri sana kwa akili yangu.”

Saa 7.30 mchana

“Pindi niingiapo kwenye chumba cha kubadilishia nguo naongea na wachezaji wenzangu, navaa jezi zangu na baada ya hapo naruka kamba kwa dakika 10 maka 15 mpaka tunapoanza kwenda uwanjani kupasha, huwa kwa kawaida dakika 40 kabla ya mechi kuanza.

Saa 9

“Huwa sina mazingaombwe yoyote kabla ya mchezo - kwangu mimi kitendo hicho ni udhaifu wa akili. Huwa nakuwa nimeipumzisha akili na kuweka umakini uwanjani tu. Soka ni kama gofu - inabidi uweke umakini lakini akili yako iwe huru, vinginevyo huwezi kucheza vizuri.

No comments:

Post a Comment