ALIYEKUWA makamu mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema
anawashangaa watu wanaomuhusisha na vitendo vya kuihujumu timu hiyo katika michezo yake ya Ligi Kuu inayoendelea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaburu aliyejiuzulu wadhifa wake katika klabu ya Simba hivi karibuni alisema watu wanaomshutumu kuihujumu Simba wana nia ya kumchafua na kumgombanisha na Wanasimba wenzake bila ya sababu za msingi.
"Wachezaji wote waliosajiliwa na Simba ni mali ya klabu ya Simba na wanalipwa mishahara na klabu hiyo na sio mtu binafsi.
"Watu wanashindwa kujiuliza baada ya kuchukua ubingwa msimu uliopita Simba imewapoteza nyota wake Kelvin Yondani, marehemu Patrick Mafisango na Emmanuel Okwi, Je? nafasi zao zimezibwa na nani?, wanatakiwa kujiuliza hivyo na siyo kuchafua watu wengine.
"Tatizo la Simba lilikuwa katika safu ya ulinzi, lakini
halikuzibwa, wamemuuza Okwi, nafasi yake haikuzibwa sasa leo watu watasema wachezaji wanatumika kuhujumu timu hiyo siyo kweli, sababu ni mapengo ya baadhi ya wachezaji hayakuzibwa,"alisema Kaburu.
Alisema yeye bado ni mwanachama halali wa Simba na ataendelea kutoa michango yake kama mwanachama na endapo atachaguliwa katika kamati yoyote yupo tayari kwa sharti la kumalizika kwa matatizo yaliyopo katika klabu hiyo kwa sasa.
Hivi jamani 2we wakweli kwan hata kumpangia mwalimu kikos haiwezi kuwa moja ya hujuma?na kama ndy kaburu aliyafanya haya kipindi cha milovan.
ReplyDelete