UONGOZI wa Simba umeamua kujivua rasmi ubingwa wao na sasa wameamua
kuelekeza nguvu zao katika nafasi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara
ambayo inaelekea ukingoni.
Simba ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi
jana umetamka rasmi kushindwa kutetea taji hilo na kuziachia Yanga na
Azam ambazo zinafukuzana kuwania ubingwa huo.
Ofisa habari wa Simba,
Ezekiel Kamwaga amethibitisha hilo na kudai kuwa kwa sasa uongozi wa
klabu hiyo wanajitaidi kuakikisha Simba inamaliza ligi ikiwa nafasi ya
pili na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mashindano ya Kombe la
Shirikisho (CAF) mwakani.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana na
mwenendo wa timu yao kwa hivi karibuni na kupelekea kushika nafasi ya
nne katika msimamo wa ligi.
''Ni kweli kwa sasa hatuwezi tena kutetea
ubingwa wetu. Kilichobaki ni kupigana kumaliza katika nafasi ya pili
kucheza Kombe la Shirikisho mwakani."
Kamwaga alisema kwa sasa uongozi wa timu hiyo una changamoto nyingi ikiwemo
usajili ya mambo mengine mengi.
No comments:
Post a Comment