WAKATI ujumbe kutoka Shirikisho la Soka Dunia (FIFA) utatua nchini
Aprili 16 kwa ajili ya kufanya tathmini ya mchakato wa uchaguzi,
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), Muhidin Ndolanga
amesema atahakikisha anaanika madudu yote yaliyofanywa na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF).
Ndolanga aliyasema hayo jijini Dar es Salaam na
kusisitiza kuwa sio yeye peke yake ambaye atakuwa mstari wa mbele
kueleza madudu ya shirikisho hilo kwani wapo wengi.
"Mimi najua wapo
watu wengi tu ambao wataenda kueleza yaliyotokea mpaka tukafika hapa
tulipo, FIFA hawana wanachokijua watataka kujua ukweli kutoka kwetu,
sisi kama wadau tutasema yetu na TFF nao watasema yao."alisema Ndolanga
ambaye ni mjumbe wa heshima wa shirikisho hilo.
“Haiwezekani TFF
ifanye madudu katika utendaji wake na bado itegemee watu wakae kimya.
Yaani dhambi na dhuluma ziachwe hivihivi, ukiuliza Fifa, mara Fifa
watatufungia, mara fifa hivi, ...,” alisema Ndolanga ambaye enzi ya
utawala wake kilichokuwa Chama cha Soka (FAT), Tanzania kiliwahi
kufungiwa kwa sababu ya serikali kuingilia kati utendaji wake.
Wakati
Ndolanga akisema hayo kuna habari kutoka kwa kiongozi mmoja mwenye
wadhifa mkubwa TFF amebainisha kuwa mgombea wa nafasi ya urais Jamali
Malinzi ana nafasi finyu ya kurejeshwa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa
kile walichoeleza kuwa amefanyiwa hujuma na klabu yake ya Yanga ambayo
ilimuandikia barua ya kielelezo kuwa ameongoza Yanga kwa miaka miwili.
"Ni
kweli kabla ajawa katibu wa Yanga alikuwa seneta na baadae katibu,
lakini hakuna na kielelezo chochote ambacho kilionyesha zaidi ya barua
ya katibu wa Yanga Laurance Mwalusako ambayo ilitanabaisha aliongoza
Yanga miaka miwili.
"Alafu hata mkoa wa Pwani hakupeleka kielelezo
kuwa anaongoza kamati ya mashindano wala mkoa wa Dar es Salaam
vidhibitisho hiyo havikuwepo sasa kama Malinzi anaweza
hakikishe anapata vielelezo hivyo vyote itakapokuja FIFA awe navyo."
alisisitiza.
Unaweza kujiuliza hapo TFF kunani?kila anayeingia hapo baada ya muda anakuwa Nunda ukimgusa tu "Ooo FIFA watatufungia".Tuliyaona hayo enzi zako mzee Ndolanga, waliokufuatia wanayarudia yaleyale utafikiri filamu/maigizo!! Hata hivyo wameyakoroga tunakuunga mkono, walipue tu kwa faida ya soka letu - mdau.
ReplyDeleteFIFA wanakuja specifically kwa ajili ya matatizo yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi na sio kusikiliza umbea.FIFA Wamekaa na Tenga kwa miaka nane na wanajua nini amekifanya katika uongozi wake na nini Ndolanga alikifanye katika uongozi wake wa kibabe wa miaka 12 pale FAT.Katika uongozi wa Ndolanga barua za FIFA zilikuwa zinatumwa kwa anuani ya ofisi yake binafsi pale Raha Towers ili wengine wasizione lakini kipindi hiki cha Tenga mambo yote yanafanyika ofisi za TFF ndio maana hata kina Michael Wambura WANAPATA NAFASI YA KUCHUNGULIA KILA MAWASILIANO YANAYOTOKA fifa KWENDA tff kwa kutumia vibaraka wao walioko TFF,enzi za Ndolanga hii isingewezekana.
ReplyDeleteHIVI HUO UCHAFU NDOLANGA AMEUONA SASA HIVI BAADA YA KUSIKIA FIFA WANAKUJA?ALIKUWA WAPI KUSEMA KABLA?MAANA HATA KAMA NDOLANGA ATAWAPA FIFA UMBEA HUO HAITASAIDIA SABABU TENGA ANAONDOKA MADARAKANI LABDA KAMA NIA NI KUMCHAFULIA TENGA KWENYE NYADHIFA ALIZONAZO KULE CAF NA FIFA AMBAZO NDOLANGA HAKUWAHI KUZIPATA KWA MIAKA YOTE 12 YQA UONGOZI WAKE FAT. TUKUMBUKE NDOLANGA ALIWAHI KUMFANYIA FITNA KAMA HIZI EL MAAMRY
ReplyDelete