Mchezaji wa zamani wa Nigeria ambaye alivichezea vilabu vya Derby County, Plymouth na Inter Milan Taribo West ametuhumiwa kudanganya ukweli kuhusu umri wake.
Mchezaji huyo aliyestaafu kwa sasa alijiunga na timu ya Serbia Partizan Belgrade mwaka
2002 baada ya kuondoka Derby County aliwaambia mabosi wa klabu yake mpya kwamba ana miaka 28.
Lakini sasa raisi wa zamani wa Partizan Belgrade, Zarko Zecevic, amemtuhumu mnigeria huyo, akisema wakati huo tayari alikuwa na umri wa miaka 40.
Taribo West wakati akiichezea Derby
'Alijiunga nasi akisema ana miaka 28. Baadae tukagundua ana miaka 40, lakini bado alikuwa anacheza soka vizuri hivyo sijutii kuwa nae kwenye timu yangu,' alisema Zecevic.
Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Croatia, mlinzi huyo ambaye alikuwa maarufu kwa nywele zake zilizojaa rangi pia alidanganya umri wakati anajiunga na timu ya Croatia Rijeka.
Akiwa na miaka 44, wanasema West alimwambia daktari wa timu ana miaka 32.
Ilikuwa ni baada ya vipimo vya afya, madaktari wakagundua kwamba magoti yake yalionyesha ni mtu mzima sana tofauti na alivyokuwa akisema mwenyewe.
Hivyo hakuweza kusajiliwa na timu hiyo lakini baadae akaenda kujiunga na Plymouth na baadae akaenda kujiunga na timu ya Iran Paykan FC mahala ambapo alimalizia soka lake akiwa na umri wa miaka 46 mwaka 2008.
Lakini leo hii ukifungua mtandao wa Wikipedia anajieleza kuwa na miaka 39.
No comments:
Post a Comment