Search This Blog

Thursday, April 4, 2013

LEO MESSI KUIKOSA MECHI YA MALLORCA: APATA JERAHA LILOMUWEKA NJE WIKI TANO MIAKA 5 ILIYOPITA

Madaktri wa klabu ya Barcelona wamesema kwamba mshambuliaji Lione Messi amepata majeraha ya misuli ya nyuma ya paja inayounganisha na hips na kwa hakika hatoweza kucheza kwenye mechi ya la liga dhidi ya Mallorca, huku uwezekano wa kurudi uwanjani baada ya hapo ukitegemea na maendeleo y uponaji wa jeraha hilo.

Jeraha kama hili alilipata miaka mitano iliyopita
Mara ya mwisho Messi amepata majeraha ya misuli ya paja ilikuwa ni March 4th 2008 dhidi ya  Glasgow Celtic katika mechi ya pili ya robo fainali ya Champions League na baada ya hapo alikaa nje kwa wiki tano.

Mara ya mwisho kuumia jeraha la misuli ilikuwa November 2009 kwenye mchezo dhidi ya Athletic Bilbao alipoumia msuli wa paja lake ya kushoto ambapo ilimbidi kukosa mchezo uliofuatia wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Inter - ingawa Barca wakashinda 2-0 mwishoni. Pia alikuja kuumia tena wakati akiwa na timu ya taifa lakini hakuweza kukosa mchezo wowote wa Barca. 

Miaka saba bila kutolewa wakati wa mapumziko
Messi alitolewa wakati wa mapumziko kwenye mechi dhidi ya PSG - ikiwa ni mara ya kwanza yeye kutolewa wakati wa mapumziko tangu February 5th 2006 katika mechi dhidi ya Atletico Madrid pale  Camp Nou, wakati kocha wa wakati huo Frank Rijkaard alipomuingiza Giuly na Ezquerro akiwatoa Messi na Van Bommel, wakati Barca wakiwa nyuma ya goli moja lilowekwa kimiani na Fernando Torres.
Leo Messi alipost hii picha na kuwaambia mashabiki wake wa mtandao wa Facebook kwamba hajaumia sana

No comments:

Post a Comment