Search This Blog

Thursday, April 4, 2013

PAPISS CISSE: KUTOKA KUWA DEREVA WA GARI LA KUBEBA WAGONJWA MPAKA KINARA WA MABAO NEWCASTLE

Aliwahi kuwa dereva wa gari la kubebea wagonjwa kwenye dharula nchini kwao Senegal.

Lakini sasa Newcastle inamhitaji na kumtegemea Papiss Cisse kuwasaidia kuiokoa timu hiyo msimu huu.
Mshambuliaji huyo leo atakuwa anaiongoza Newcastle kwenye dimba la Estadio da Luz kwenye robo fainali ya kombe la UEFA.

Ushindi dhidi ya Benfica kwenye robo fainali itamfanya Alan Perdew na vijana wake kuzidi kuusogelea ubingwa wao wa kwanza tangu walipobeba ubingwa wa Fairs Cup in 1969 ukiutoa wa Intertoto Cup 2006.
Lakini pia itawapa ahueni na matumaini ya kuepeuka kushuka daraja kutoka kwenye Premier League.
Newcastle wana pointi 3 zaidi kutoka kwenye ukanda wa timu zitakazoshuka daraja baada ya kubamizwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi Manchester City.
Na ving'ora vya hatari vimeanza kulia pale ST. James Park. 

Lakini Cisse si mgeni wa ving'ora kwa sababu tayari alishakuwa mfanyakazi wa gari la kubebea wagonjwa kwa dharula tangu akiwa na umri wa miaka 15. 

Kwa sasa anamiliki kituo cha hisani na ameweza kukusanya fedha za kutosha kununua ambulance mpya, X-ray machine na vifaa vingine vya matibabu kwa ajili ya Hosptali yake huko kwao Senegal. 

Muda mchache kabla ya kwenda Lisbon, SunSport ilimfanyia surprised Cisse kwa kumpelekea gari la analolijua kiundani - linalomilikiwa na North East Ambulance Service Foundation Trust. 

Na mshambuliaji huyo mwenye thamani ya £10million anakiri kumbukumbu za kazi yake ya zamani zilimrudia kwa kasi sana mara baada ya kukaa kwenye usukani mwa gari hilo.

Anakumbuka: “Wakati nakua kule Sedhiou hospitali haikuwa na vifaa vya ubora.
“Hivyo nilikuwa nawachukua watu kutoka kijijini kwetu kwenda mji mwingine, Dakar, ambapo kulikuwa na Hosptali bora zaidi.

“Nilikuwa nawaendesha wagonjwa kwa umbali wa masaa matatu mpaka manne kwenye ambulance.
“Na kwa bahati mbaya niliweza kushuhudia vifo vingi njiani kwa sababu hawakuweza kuhimili mpaka kufika hosptali. 

“Kulikuwa na kesi nyingi za wanawake ambaye walipata kupoteza watoto kutokana na mimba zao kuharibika na wengine wakipoteza maisha safarini.
“Hilo ni jambo ambalo linaloniumiza sana kila nikikumbuka.
“Ikiwa na nina jukumu binafsi kwenye maisha yangu ni kusaidia hosptitali kwenye mji wangu.

“Nataka watu wengi wawe na vitendea kazi vyote ili waweze kuwashughulikia wagonjwa mahala pale pale wanapoishi."
Cisse, 27, anaendesha taasisi ya Friends of Sedhiou kutoka nyumbani kwao kusini mashariki mwa Senegal - na pia kwa sasa ana mahusiano ya kimapenzi na Miss Newcastle 2012, Rachelle Graham.
Ni miezi 15 tangu alipowasili kutoka Freiburg na akaenda kufunga mabao 13 kwenye mechi 14 kuisadia Newcastle kushika nafasi ya 5. 

Ingawa msimu huu amekuwa na ukame kiasi, goli lake la umbali wa 20-yard dhidi ya Southampton na kufuatia na mabao ya ushindi ya Stoke City na Anzhi Makhachkala iliwakumbusha mashabiki uwezo wake wa kuwafanyia ugaidi mabeki wa timu pinzani. 

Cisse anapenda maisha ya kaskazini mashariki mwa Uingereza. Alikiri: "Najihisi nipo nyumbani. Nimekaribishwa vizuri tangu nilipofika hapa.
“Mashabiki wa hapa ni maalum sana na watu wa aina yake sana.
“Muda mwingine unaweza ukakutana nao mitaani na ni vizuri kuwa ninaongea nao - hainigharimu chochote kufanya hivyo na jambo hilo linanifurahisha sana.
 
“Miezi yangu sita ya kwanza hapa nimekuwa na furaha sana uwanjani na maisha yanguya nyumbani. Kila ninachokigusa kinageuka dhahabu.

“Sasa hivi nimekuwa na ukame kiasi kwa sababu mabeki wameshaanza kunikamia lakini najitahidi kufanya sana mazoezi ili niwe fiti zaidi niweze kurudi kwenye form niliyokuwa nayo msimu uliopita."
Cisse kwa sasa ndio mshambuliaji tegemeo wa toon tangu Demba Ba ajiunge na Chelsea mwezi January.
Takwimu zinaonyesha wasengali hawa hawakung'ara kwa pamoja kwenye dimba la St. James Park kitu ambacho kiliwafanya mashabiki wa Newcastle kukosa amani.
Wote walifunga kwenye mechi ya kwanza Cisse dhidi ya Aston Villa mwezi February 2012.
Lakini hilo ndio likawa goli la mwisho la Ba kwenye msimu huo — japokuwa alikuwa na msimu mzuri mwanzoni alipofungamabao 15 kwenye ligi mara tu baada ya kuhamia kutoka West Ham United.
Mara nyingine wawili hao kufunga kwa pamoja ilikuwa kwenye mechi ya ushindi wa Magpies dhidi ya Chelsea kabla ya Ba hajahamia Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment