Search This Blog

Saturday, July 28, 2012

BAADA YA KUSHUKA KIWANGO - RYAN BABEL ASHUSHWA HADI KIKOSI CHA PILI CHA TSG HOFFENHEIM

Baada ya kuonyesha kiwango kisichoridhisha kwa takribani miezi kadhaa iliyopita, mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uholanzi Ryan Babel ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya TSG 1899 Hoffenheim inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Bundesiliga ya Ujerumani - ameshushwa kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha klabu hiyo ilipanda daraja mwaka 2008 na kushika nafasi ya pili kwenye bundesiliga.


Kwa taarifa nilizozipata leo kutoka kwa kocha msaidizi wa TSG Hoffenheim, Rainer Widmayer ni kwamba baada ya manager wa klabu hiyo Markus Babbel kuona kiwango cha mchezaji huyo kikizidi kushuka amemshusha kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha timu hiyo, huku akiwekwa sokoni kwa kuuzwa kwa €5 million, lakini amekuwa hana soko.


HII NDIO INTERVIEW NILIYOFANYA NA KOCHA TSG HOFFENHEIM

No comments:

Post a Comment