Mpendwa RVP
Ningependa kukupongeza kwa kuwa msimu mzuri uliokuwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Ulimaliza msimu bila kupata majeruhi, ukishinda tuzo nyingi, na kuvunja rekodi za klabu na ligi kuu; kitu ambacho kitaenda katika vitabu vya historia ya Arsenal.
Ulileta utulivu, amani na heshima kwenye kikosi ndani na nje ya uwanja.
Mtu mkubwa, mwenye majukumu mazito; Ulitekeleza majukumu yako vizuri, tena vizuri zaidi ya vile nilivyotegemea.
Kama mshabiki wa Arsenal, Nimeshuhudia vipaji vingi na ninakiri, umebarikiwa sana na ninadiriki kukuita "genius".
Lakini, tarehe 4 ya mwezi July 2012, ulishusha bomu ambalo limeigeuza Arsenal kuwa sehemu iliyochafuka, ulipotoa taarifa iliyoelezea nia yako ya kutosaini mkataba mpya ambao klabu ilikuwa imekupa.
Mimi ni nani kukuambia cha kufanya? Lakini najua kitu kimoja kwa hakika, Arsenal ilikuwa Arsenal, Arsenal ni Arsenal, na itaendelea kuwa Arsenal.
Watu wengi wamekuwa wakitushambulia kwa kukosa tamaa ya mafanikio, jambo ambalo silipingi, lakini kwa kipindi hiki cha usajili tumekuwa wepesi sana katika kusajili, tayari tumemsajili Lukas Podolski na Olivier Giroud.
Nimekuwa nikiamini ilikuwa step iliyokuwa na mweleko mzuri, kuwasajili wachezaji ambao tayari wameshathibitisha kuwa ni daraja la juu ili kuweza kukupunguzia mzigo wewe uliokuwa nao msimu uliopita.
Pamoja na kuwa nyuma kwenye nafasi ya tatu, lakini tuliweza kufuzu kushiriki kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya msimu, huku tukivishinda vilabu vilivyotumia fedha nyingi kwenye usajili kama Liverpool, Tottenham na Chelsea ambao wamefuzu kwa sababu tu walikuwa mabingwa wa ulaya.
Umekuwa kwenye klabu hii kwa miaka nane sasa, naweza kusema nimekushuhudia dimbani kwa misimu miwili tu. Katika misimu hii miwili ulikuwa unacheza vizuri kabisa, ukifunga magoli muhimu na mazuri.
Misimu sita iliyobaki ilikuwa imejaa na kuandamwa na majeruhi, majeruhi na majeruhi zaidi ambayo mwishowe yalikupa jina ya "The Man of Glass".
Wakati ukiwa kwenye nyakati ngumu za maisha yako ya soka, kipindi ambacho baadhi ya mashabiki walitaka uondoke, unadhani nani alikusimamia pale? Arsene Wenger! Sasa fikiri angekubalina na matakwa ya mashabiki waliotaka uondoke, ungekuwa kama alivyo Alberto Aquilani sasa hivi.
Kama ninavyopenda kukupongeza juu ya kiwango chako msimu uliopita, pia naamini kulikuwa na kitu kilichoitwa "teamwork".
Haikuwa tu teamwork, kilikuwa ni kikosi chote cha Arsenal kikicheza kama familia. Umoja ndani ya kikosi ulikuwa na nguvu, wachezaji wenzio walikuwa tayri kufanya lolote kwa ajili yako.
Kama unakumbuka mchezo dhidi ya Wigan katika uwanja wa DW stadium ambapo tulitoka na ushindi wa 4-0, Theo Walcott alikuwa na nafasi ya kufunga, lakini alichagua kuchelewesha mpira, kabla ya kukupa wewe assists na ukafunga huku ukizidi kujiongezea wastani mkubwa wa magoli ya kufunga.
Kila mtu alitaka ufanikiwe.
Namuangalia Wayne Rooney na Antonio Valencia, najiuliza ni mara ngapi nimeshuhudia wanavyosadiana dimbani, ushirikiano na umoja wa wachezaji ni kitu ambacho fedha haiwezi kununua.
Mfano mzuri tumehushudia hivi karibuni kwenye michuano ya Euro 2012 iliyomalizika hivi karibuni, alikuwa wapi yule Van Persie wa msimu uliopita wa Arsenal?
Sasa tamaa yako ya mafanikio imekuwa sana kuliko ya klabu ndani ya msimu mmoja mzuri?
Wapi ilipokuwepo tamaa yako ya mafanikio mwezi uliopita mlipotolewa kwa aibu kwenye Euro 2012, ilikuwa wapi tamaa yako ya mafanikio kipindi Arsenal wanakutibia majeraha yako kwa miaka, ilikuwa wapi tamaa yako ya mafanikio ulipokuwa ukipokea pesa nyingi kwa kazi usioifanya?
Muda wa kuilipa fadhila Arsenal kwa imani waliyoinyesha kwako, tamaa yako ya mafanikio ghafla imekuwa kubwa?
Sikulaumu sana wewe, Namlaumu Arsene Wenger.
Imani yake isiyokufa na mapenzi yake kwa wachezaji kama Matheieu Flamini, Samir Nasri, Gael Clichy, Cesc Fabregas na wengine, ndio inayomponza.
Gianfranco Zola alikuwa moja ya wachezaji waliobarikiwa vipaji vikubwa ambao wamewahi kuonekana kwenye premier league. Alipata mafanikio gani na Chelsea? Lakini jina lake litaendelea kubaki kule juu kama gwiji kila aina ya maneno unayoweza kuyatumia.
Mwisho, ningependa kukushukuru kwa muda mzuri uliotuletea hapa, magoli mazuri uliyofunga(sina idadi kamili).
Nakutakia mafanikio mema kwenye maisha yako ya soka, nakutakia mafaniko kwenye klabu yako mpya. Nenda kashinde makombe ndugu.
Pindi utakapoondoka nakuomba unifanyie jambo moja, sahau kila kitu kuhusu Arsenal na tafadhali usijaribu kutuzungumzia.
Badge iliyopo kwenye jezi pembeni mwa kifua siku zote itakuwa kubwa na thamani kuliko jina lililopo nyuma.
Kwaheri RVP

Imeandikwa na shabiki wa Arsenal.
Daaaaahhhhhhhh nimeamini huyu ndio mshabiki wa kweli Arsenal pole kk najua unamachungu sana bt haina jinsi.
ReplyDeleteMuache aende! Hakucheza kwa kiwango Henry baada ya kuondoka Arsenal sembuse yeye. Kama ni vikombe anataka atavishangilia akitokea benchi. Sikumbuki sawasawa kama kuna mchezaji aliyehama Arsenal akaenda kuwa na makali yaleyale isipokuwa Cesc ndiyo amefanikiwa kwa kiasi fulani. Ni mtazamo wangu. Unaweza kuwa wa kishabiki zaidi lakini ndiyo ninachokiami.
ReplyDeleteNafikili asilaumiwe sana kwa uamuzi alio fanya naye yupo ktk mchakato wa kutafuta maisha mazuri, matibabu ni haki yake. Mbona kuna watu wamesomeshwa na fedha za wananchi nabado hawawathamini na kuamua kuwaibia fedha zao walizokabiziwa wazitumie kuwasaidia wananchi kuboresha maisha yao. I hope anastahili kuombewa mafanikio mema aendako japo inauma no way out, kila la kheri kaka.
ReplyDelete