Search This Blog

Friday, May 4, 2012

HILI NDIO GOLI BORA KATIKA MISIMU 20 YA PREMIERLEAGUE - ROONEY AFUNIKA



 Goli la Wayne Rooney la tik taka dhidi ya Manchester City msimu uliopita limeshinda kama goli bora kabisa tangu kuanza kwa Barclays Premier League - kwa maana ya msimu 20 iliyopita.

Bao hilo lilitangazwa jana alhamisi jioni na chama cha waandishi wa habari wa soka katika chakula cha usiku jijini London.

Wayne Rooney akiwa na tuzo yake.


Mshambuliaji huyo wa Manchester United  alifunga bao hilo katika uwanja wa  Old Trafford mwezi wa pili mwaka jana limeyashinda magoli mengi yaliyofunga katika miongo miwili iliyopita.



Maelfu ya wapenzi wa soka duniani walihusika katika kupiga kura - huku Rooney akipata asilimia 26 ya kura zote, goli la Dennis Bergkamp dhidi ya Newcastle akiwa na Arsenal mwaka 2002 lilishika nafasi ya pili, huku goli la Thierry Henry dhidi ya Manchster United mwaka 2000 likishika nafasi ya tatu.

1 comment:

  1. Nafikiri ni goli ambalo limestahili kupata tuzo, lilikosa tuzo kwenye FIFA ila kuingizwa kwake kule kulimaanisha kuwa lilikuwa goli bora pia.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete