Search This Blog
Friday, November 22, 2013
BAYERN MUNICH VS DORTMUND: KLASSIKER YA KWANZA YA MSIMU HUU WA BUNDESLIGA - DORTMUND WAKIWA NA HALI MBAYA YA MAJERUHI
Inaweza kuwa haina ukubwa wa El Clasico ya Spain, lakini katika miaka ya hivi karibuni Borussia Dortmund na Bayern Munich wamejenga upinzani mkubwa unaoifanya mechi baina yao iwe miongoni mwa mechi 'classics'. Hivi sasa mechi hiyo imepewa jina Bundesliga Klassiker, na jumamosi hii itakuwa ndio klassiker ya kwanza itakapochukua nafasi.
Japokuwa ni bado kabisa mwanzoni mwa msimu mpya, lakini matokeo ya mechi hii yatatokea muelekeo wa ubingwa utaelekea wapi msimu huu, ubingwa ambao Bayern waliuchukua kutoka kwa Dortmund msimu uliopita.
Baada ya Jupp Heynckes kuiongoza Bayern kushinda makombe matatu msimu uliopita, Pep Guardiola tayari ameanza vizuri. The Bavarians wamedondosha pointi 4 tu kutoka katika michezo yao 12 na tayari wanaongoza ligi kwa pointi nne mbele ya Dortmund na Bayer Leverkusen.
Bayern chini Guardiola pia wana rekodi nzuri. Chini ya filosofia za Pep ina maana sasa Bayern wana uwezo wa kumiliki mpira zaidi huku wakifanya 'pressing' kama msimu uliopita, mbinu ambayo Dortmund wanaimudu pia.
Kitu kingine cha kuvutia kuhusu kuanza vizuri kwa Guardiola ni kwamba amekuwa akiandamwa na majeruhi katika kikosi chake , hasa kwenye kiungo. Thiago Alcantara, Bastian Schweinsteiger, Javi Martinez na Mario Gotze wote wamekuwa wakikosekana kwenye mechi za msimu huu, lakini Guardiola aliweza kuimudu hali hiyo vizuri sana. Uamuzi wa kumhamisha kutoka beki wa kulia Philipp Lahm mpaka kwenye kiungo umeonyesha kuwa na mafanikio jambo ambalo lilipelekea hata kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low kumtumia kwenye eneo hilo wiki iliyopita.
Wakati Thiago, Martinez na Gotze wakiwa wamerudi kwenye uzima, Schweinsteiger kwa mara nyingine atakosekana kwenye mechi ya kesho na ataungana na majeruhi wengine kama Frank Ribery aliyeumia kwenye mechi ya kugombea kufuzu michuano ya kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa. Kutokuwepo kwake kunaongeza nafasi ya kuanza kwenye mechi itakayochezwa kwenye dimba la timu ambayo imemtambulisha vizuri kwenye ulimwengu wa soka.
Kuondoka kwa Gotze Dortmund kunaonyesha wazi pengo la rasimali baina ya vilabu hivi vikubwa viwili, jambo ambalo linaonyesha wazi ukubwa wa mafanikio ya timu hiyo nyumbani na ulaya katika miaka ya hivi karibuni. Jurgen Klopp anakutana na changamoto kubwa ya kuendelea kuiongoza kwa mafanikio klabu hiyo kama msimu uliopita. Kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri, mpaka katika michezo miwili iliyopita walipofungwa na Arsenal nyumbani na kuweka hatma yao katika Champions league kuwa shakani kabla ya kufungwa na Wolfsburg jambo ambalo linamaanisha itabidi waepuke kufungwa jumamosi ikiwa wantaka kubakia kuwa washindani wa ubingwa wa Bundesliga.
Kama ilivyo kwa Bayern, Dortmund wamekuwa wakiandamwa na matatizo ya majeruhi msimu huu, lakini tofauti na wapinzani wao, wenyewe wanakosa kikosi imara bila kuwa na wachezaji wanaowategemea. Kiungo wao tegemezi Ilkay Gundogan amecheza mechi moja tu msimu huu kutokana na majeruhi, pia kwa bahati mbaya zaidi katika mechi dhidi ya Bayern Jurgen Klopp itabidi apange kikosi ambacho kitakuwa hakina mchezaji hata mmoja wa kikosi cha kwanza katika safu ya ulinzi.
Lukasz Piszczek bado hajacheza kabisa msimu huu, wakati beki wa kati Neven Subotic amepata tatizo la goti katika mchezo dhidi ya Wolfsburg. Kama hilo halitoshi, wote wawili Mats Hummels na Marcel Schmelzer wakaumia katika mechi za kimataifa wiki hii mwanzoni. Beki mkongwe wa kijerumani Manuel Friedrich amechukuliwa kwa mkopo wa muda mfupi na anaweza kuanza kwenye mechi ya kesho.
Dhidi ya safu kali na bora ya ushambuliaji ya Bayern, itawahitaji kuwepo kwa juhudi kubwa zaidi kutoka kwenye safu ya ulinzi ya Dortmund ili kutoka japo na sare kwenye mchezo huo. Dortmund walishinda kwenye mechi yao ya kwanza waliyokutana msimu huu katika German Super Cup, lakini hiyo ilikuwa wakati Guardiola alipokuwa akitafuta baance ya timu. Ni vigumu kuona matokeo yanayofanan jumamosi ya kesho na Bayern wanaweza kupiga hatua kubwa kuelekea kwenye ubingwa wa Bundesliga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment