Search This Blog

Thursday, November 21, 2013

KASEJA APIGWA CHINI KIKOSI CHA STARS CHALLENJI: IVO, DILUNGA, KIMWAGA, SAMATA NA ULIMWENGU NDANI

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.

Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu.   

MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE YAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 3,682,560.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 5,928,124, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,976,041.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.


8 comments:

  1. Huo ni umbea inamaana hauwezi kuwa na Title nyengine zaidi ya hiyo!nani asiye jua kama kaseja ametemwa kwa kutokuwa na timu.unaandika kama mwandishi wa gazeti kusema uuze.


    kuntah kinte.

    ReplyDelete
  2. nakupongeza mchangiaji wa kwanza.. kim alisema kaseja bado ni nahodha and akipata mechi ataitwa tena... mbona tangu mwanzo tulijua hayupo coz ata mechi ya stars na future young stats hakuwepo?? au hujui hao walioteuliwa mchakato ulianzia wapi?? poor choice of tittle

    ReplyDelete
  3. Dilunga ni fundi ila ajitunze

    ReplyDelete
  4. bora ungesema Barthez sio kaseja babu hebu rekebisha.

    ReplyDelete
  5. timu nzuri niwakati wao kuonyesha vipaji ,kuchukua challange ni ngumu lakini tukifika hata robo final inatosha san inacho itajika ni wao wachezaji kutumia vizuri maelekezo ya mwalimu .kwa maoni yangu mimi mabeki wote wasitoe pasi za mwisho, pasi hizi za mwisho zitolewe na midfield's tu ,tunataka kuona raha ya mpira hii itawafanya mabeki kujiamini na kutobutua butua mipira ovyo.

    ReplyDelete
  6. Kaseja yake yamepita tutazame mengine

    ReplyDelete
  7. Kaseja hata mwalimu kasema hawezi kumtumia kwa kuwa hana timu sasa sijui kuna nini mpaka iwe anabaeba khabari kila siku nadhani kuna wadau baadhi yao wana maslahi binafsi na kaseja ndio maana amekuwa anabeba vichwa vingi vya khabari watanzania tunatakiwa kukumbuka kuwa tulikuwa na makipa zaidi ya kaseja mara ngapi sidhani kama kaseja kawafikia hao akina omar mahadhi kina mambo sasa kina idi pazi kina mwameja khamis kinye na wengineo kaseja wa kawaida sana asiwe gumzo kiasi hiki jamani tuna deni kubwa katika soka letu sio kaseja

    ReplyDelete