Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya Kili
Nani Mtani Jembe itaendelea kuunguruma tena Jumapili wiki hii na kuwapa nafasi
mashabiki wa Simba na Yanga walioko Dodoma, Musoma na Singida na kuchuana
vikali katika michezo mbalimbali huku wakihakikisha timu zao zinaibuka na kitita
cha shilingi milioni mia moja zilizotengwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa
ajili ya Watani wa Jadi kupitia kampeni hiyo.
Mratibu wa mabonanza hayo, Lawrence Andrew amesema jijini
Dar es salaam jana kwamba mashabiki watapata fursa ya kushiriki katika michezo
mbalimbali kama vile foosball, kuvutana kamba, soka la wachezaji saba kila
upande maarufu kama “Seven aside” na kuongeza kuwa ili kuhakikisha mashabiki
hao wanafurahia ipasavyo burudani mbalimbali za muziki zitakuwepo pamoja na
Nyama choma.
Andrew alisema kuwa
katika mji wa mji wa Dodoma bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika
uwanja wa shule ya Dodoma Sekondari ambapo bendi maarufu ya The TNC Band
itatumbuiza. Na huko Musoma bonanza litafanyika katika uwanja wa Mukonde na
kupambwa na bendi ya Musoma Stars huku mkoani Singida likifanyika katika
Uwanja wa Namfua na burudani kabambe ikishushwa na Wana Pamba Music Band aka
Watoto wa Mujini bendi ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana mkoani humo.
Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya
kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga
penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba mabonanza hayo ambayo yatafanyika
katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia Nani Mtani Jembe. Kampeni hii ya aina
yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika
na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao
huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni
mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo inafanyika nchi nzima
ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni
hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga
kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila
timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa
mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni
hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu
nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka
kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la
Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni
kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba
ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona
namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani
na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha
anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki
aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000
kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha
zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa
shindano hilo Desemba 14, mwaka huu siku ambayo watani wa jadi Simba na Yanga
watacheza mechi ya kuhitimisha kampeni hiyo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam.
No comments:
Post a Comment