Ian Wright na Van Persie |
Mholanzi huyo ambaye alikuwa nahodha wetu ameenda Old Trafford kwa sababu anaamini kuichezea United kutampa nafasi nzuri zaidi ya kushinda makombe.
Na hili linatuumiza mashabiki wa Arsenal.
Van Persie alijiunga na Gunners mwezi May 2004, muda mchache baada ya klabu yangu ya zamani kumaliza msimu bila kufungwa katika ligi kuu ya England.
Hii ilikuwa timu bora kabisa ya Arsenal. Ilikuwa na uwezo wa kuendelea kutawala kwa misimu mingi zaidi.
Lakini, mwaka baada ya mwaka, wachezaji wakubwa waliondoka.
Jens Lehman, Ashley Cole, Sol Campbell, Robert Pires, Thierry Henry na Patrick Vieira wote wakaondoka.
Na tangu awasili kutoka Feyenoord, Van Persie aliweza kushinda kombe moja tu - FA Cup, miaka saba iliyopita.
Ni aibu kubwa kuona mholanzi huyu akiwa anaungana listi ndefu ya wachezaji wazuri kuondoka Arsenal, ingawa haijanishangaza. Kama mashabiki wa Arsenal wanakuwa wakweli wa hisia zao, naamini hawatokuwa wameshutushwa pia. Ni dalili za wakati mbaya.
Timu tatu ambazo siku zinaonekana kuweza kushinda makombe ni United, Man City, na Chelsea.
United hawakushinda chochote msimu uliopita na baadhi ya watu wanasema Alex Ferguson alikuwa na kikosi kibovu kuliko vyote katika historia ya kuifundisha United.
Lakini bado walipoteza kombe lao kwa tofauti ya magoli katika dakika za mwisho za ligi.
Kwa hakika mambo yatakuwa tofauti msimu wa 2-12/13, kama ambavyo imekuwa ni vigumu kwa United kumaliza msimu bila kushinda chochote.
Sipendi na ninachukia sana kuona wachezaji muhimu wakiondoka Emirates na itaendelea kuzidi kuwa vigumu kwa klabu kuwashikilia wachezaji wao wengine muhimu.
Kumbuka, Theo Walcott anakaribia mwisho wa mkataba wake akiwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na naomba asaini mkataba mwingine mpya wiki chache zijazo.
United, City na Juventus wote walikuwa wakimtaka Van Persie lakini nafikiri amefanya maamuzi sahihi kujiunga na United.
City wapo katika kipindi cha kusisimua na wanaweza kushinda makombe mengi miaka kadhaa ijayo.
Lakini bado Van Persie ambaye ana miaka 29 ameshindwa kukataa kuichukua nafasi ya kuichezea klabu kubwa zaidi duniani. Wachezaji wakubwa wanataka kucheza na wachezaji wenzao wakubwa - na kwa hilo Van Persie amelipata kwani atakuwa na nafasi ya kufanya uharibifu mkubwa kwenye nyavu za maadui akiwa sambamba na Wayne Rooney.
Ferguson siku zote amekuwa akiongoza timu na kuwajenga kuwa na winning mentallity na Van Persie, inaeleweka anataka kuwa mmoja ya timu ya namna hiyo.
Msimu uliopita, aliibeba Arsenal. Inabidi ujiulize ni wapi tungemaliza kwenye msimu bila mabao yake 37.
Nina hisia za kumuonea huruma sana Arsene Wenger lakini, mwishowe yeye ndio anafanya maamuzi ya mwisho katika kucheza kwa mchezaji na kutoa ofa ya mkataba mpya.
Baadhi ya watu wanasema Van Persie ingebidi aonyeshe upendo zaidi kwa Arsenal, baada ya majeruhi yote ambayo aliyapata. Lakini kama nilivyosema mwanzoni, upendo wa dhati siku hizi unatoka kwa mashabiki tu na hili jni jambo ambalo itabidi likubaliwe.
Kwa kuwaondoa wachezaji kama Ryan Giggs, Paul Scholes pale United na John Terry pale Chelsea, hakuna wachezaji wanaoweza kudumu kwenye timu moja milele.
Arsenal sasa tunajikuta kwenye wakati mgumu.
Klabu imesajili washambuliaji kama Lukas Podolski kutoka Cologne, mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud kutoka Montpellier na kiungo wa Kispain Santi Cazorla kutoka Malaga, ambao wanaweza kufanya vizuri kwenye EPL.
Lakini angalia natumia neno "wanaweza".
Wenger anahitaji wachezaji hawa kucheza vizuri sana, lakini inawezekana sio jambo zuri sana kuwa na mategemeo makubwa sana kwa wachezaji hawa watatu wapya.
Nafunga mikono yangu nikiomba, wote wafanye vizuri mapema zaidi.
Mashabiki wengi wa Gunners wataangalia ratiba ya ligi na kufahamu tarehe za mechi za United.
Itakuwa pale Old Trafford november 3, ambayo itakuwa Birthday yangu, United wataikaribisha Arsenal kwenye mechi ya kwanza, kabla ya vijana hao wa Fergie hawajasafiri kwenda Emirates April 27.
Sitaki kufikiria wala kuwaza kwamba Van Persie atapata mapokezi mazuri na nina uhakika hatokuwa akitegemea kupata mapokezi mazuri.
Kwa bahati mbaya, Arsenal kwa mara nyingine tena ni lazima waendelee mbele kufuatia kuondoka kwa jina lingine kubwa klabuni.
Unaweza ukaweza nini wangefanya au wangekuwa na nini kama wachezaji wote wangebaki Emirates.
Kwaheri RVP - Nakutakia kila la kheri @Theatre of Dreams.
Imeandikwa na Ian Wright
No comments:
Post a Comment