Timu ya soka Simba B ya Dar es salaam leo imefanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza wa kombe la BancABC Super8 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mabao 4-3 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuzisalimu nyavu za Mtibwa katika dakika ya 18 kipindi cha kwanza baada ya mshambuliaji wake hatari Edward Christopher, kabla ya Shabaan Kisiga hajasawazisha dakika ya 31.
Mpaka mchezo unaisha kwenye dakika 90 timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3, na hivyo kupelekea timu hizo kuelekea kwenye dakika 120 na ndipo kwenye dakika hizo Simba wakapata bao la ushindi, na mpaka dakika 120 zinakamilika Simba 4-3 Mtibwa.
Kwa usindi huo Simba B imelamba kiasi cha millioni 40 kama zawadi ya mshindi, huku Mtibwa kama washindi wa pili wakitia benki millioni 20.
Naomba mrekebishe kauli zenu,hiki sio kikosi cha pili bali ni Simba. Kwa speed ile Yanga anakula TANO zingine maana kwa butuabutua ya Nadir Haroubu na Ubabu wa Nsajigwa watatokwa na Bandama kwa jinsi watakavyo kimbizwa na akina Edo,Messi,Sekule na wengineo. Naushauri uongozi wa Simba waachane na dhana ya wachezaji wa nje nje nibora. Msimu ujao tusisajili wachezaji wengine bali tupandishe timu nzima hii iliyocheza Super8r
ReplyDelete