Jana nilitoa nafasi kwa mashabiki wa Arsenal kuweza kutoa maoni yao juu ya suala la uhamisho wa mshambuliaji Robin Van Persie kwenda Manchester United, mamilioni ya washabiki wa Arsenal duniani walianza kuitumia kila nafasi wanayoipata kutoa maoni juu ya uhamisho huo, wengine walimtakia kheri, wengine walimkashifu na kumpa majina ya ajabu ajabu huku wengine wakijaribu hata kuchoma hata jezi zake. Kutokana na hilo nilijaribu kutoa nafasi kwa washabiki wa Arsenal ambao ni wadau wa mtandao huu kutoa maoni yao juu ya uhamisho wa Robin Van Persie. Na haya ni baadhi ya yale niliyotumiwa.
Finley Fabregas |
Habari Bw. Dauda,
Naandika maneno haya sio kwa kejeli au furaha, mie ni muanga mkubwa wa zoezi hili.
Ukija katika dawati langu la kazi nna kikombe (mug) chenye charter/log
ya washika bunduki, mwanangu wa kwanza na nnae huyo tu hadi sasa
anajulikana kwa Finley Fabregas (wakati wa ubatizo wake padre wa Kanisa
Katoliki pale Moro aligoma, lakini baadae akaelewa), namaanisha nini ?
Hapa ni kuwa RVP katutenda km ilivyokuwa mwaka jana kwa Cesc..... ila
Arsenal chini ya Mkufunzi nimwite Mchumi Mzee Arsene WENGER ni
mzalishaji kwani watatokea akina van Persie wengi tu msimu huu, na pale
ukiondoka kwa kajeli umeumia kwani wapi akina Flamini, Helb nk walikuwa
wakupotea leo la hasha..... akituuzi tutampiga majeruhu msimu mzima
(kosa lake RVP ni kwenda siko, kwa mahasimu basi).
Inshalaah guners ipo na itaendelea kuwepo, acha tuumie japo mechi 3 za awali,
Ndugu Shaffih Dauda.
Mimi kama mshabiki wa klabu ya
Arsenal ya Uingereza nimesikitishwa sana na hatua iliyofikiwa na klabu
ya Arsenal ya kumuuza mshambuliaji Robin Van Persie kwenda Manchester
United. Katika historia yote ya klabu ya Arsenal kuwa na wachezaji
wazuri na baadae kuwauza pindi wanapotakiwa na klabu nyingine lakini hii
ya kumuuza Van Persie kwenda Man United ndiyo imefunga jarada. Hii
inaonyesha jinsi gani sasa ushindani na uhasimu katika mpira wa miguu
umekwisha.. Kitu kikubwa sasa klabu kama Arsenal inajali mapato zaidi na
sio mafanikio ya klabu.Arsenal na Man United ni maadui wakubwa katika
ligi ya Uingereza mpaka ukiona viongozi wao wanakaa meza moja na
kujadiliana kuuziana wachezaji ujue sasa uhasimu umeisha watu wana jali
pesa. Je ulisha wahi sikia America waka kaa meza moja na Russia kujadili
kuuziana silaha?Je ulisha wahi sikia ati serekali ya Afganistan ika kaa
meza moja na wafuasi waTaliban kujadili kuuziana silaha? Uongozi wa
Arsenal umefanya yote mabaya lakini hili la kumuuza Van Persie kwa
wahasimu wao Man United halitasahauliwa na mashabiki wa Arsenal duniani
kote. Kila wakati timu hizi zitakapo kutana msimu huu basi vurugu
zitatokea kwa washabiki kumzomea sana Van Persie au kupigana kati ya
mashabiki watimu zote mbili.Biashara ya Van Prsie toka Arsenal kwenda
Man United naiona kama imekiuka misingi mingi ya uadui katika timu hizi
mbili. Kwa miaka mingi mashabiki wa Arsenal watamchukia sana Van Persie
kuliko wachezaji wengine waowahi kuhama kama vile
Nasri,Adebayor, KoloToure, Ashely Cole, na wengineo.
DOCTOR.
MSHABIKI WA ARSENAL, STOCKHOLM-SWE
No comments:
Post a Comment