Search This Blog
Thursday, January 2, 2014
PICHA ZA WATANGAZAJI NA WANAFAMILIA WENGINE WA CLOUDS FM WAKITOA MISAADA DSM.
Ni tukio ambalo limefanyika Jan 1 2014 ikiwa ni siku ya kilele cha shamrashamza za miaka 14 ya kuzaliwa kwa Clouds FM ambapo ikiwa ni radio ya watu na kutambua kwamba kuna wengine wanaopitia matatizo kwenye maisha yao kwa wakati huu, team nzima iliingia mtaani na kutoa misaada mbalimbali.
Misaada ilianza kutolewa kwenye hospitali ya Temeke ambapo ilitolewa kwa Wagonjwa na kwa hospitali yenyewe na baada ya hapo team nzima yenye zaidi ya watu 30 ikaelekea moja kwa moja kwenye kituo cha Keko Machungwa ambacho kinamilikiwa na kijana Yohana aliekua anatumia dawa za kulevya ambae ameacha na kuanza kusaidia wengine.
Kwenye kituo hiki ambacho kilitambua umuhimu wa maneno ‘radio ya watu’ kilipeleka maombi ya kusaidiwa mashine ya Compressor ili kurahisisha kazi ya useremala kwenye ofisi ya kituo hiki chenye waathirika 40 ambao baada ya kutibiwa wamekua wakipewa mafunzo ya useremala ili kupata kipato kwa hiyo kazi.
Team CLOUDS FM na wagonjwa hospitalini
Mrisho Mpoto ni mmoja wa Wasanii waliojitokeza kuunga mkono.
Regina Mwalekwa hospitali
Mtu wako wa nguvu kwenye wodi ya watoto
Kuanzia hii picha ya juu na hizi zinazofata ni tukiwa kwenye kituo cha Keko Youth Centre
Shamba wanalolimia mboga watu wanaosaidiwa na kituo hiki
Yohana mwenye kituo, Sebastian Maganga ambae ni mkuu wa vipindi Clouds FM pamoja na Said Fela kiongozi wa Wanaume Family.
Team Clouds ikimsikiliza Yohana
Msaada uliotolewa na Clouds FM
Sehemu ya miradi inayomilikiwa na kituo hiki cha kusaidia watu walioathirika na dawa za kulevya.
Mtu wako wa nguvu na watu wake wa nguvu mtaani, ni furaha yangu.
Hizi picha hapa chini zinazofata ndio Team Clouds ilikua inakabidhi misaada kwa hospitali ya Temeke.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Clouds mmetufundisha kitu pamoja na kutukumbusha uliowajibu wetu,Mungu awabariki sana kwa baraka za rohoni na za mwilini.
ReplyDeleteNiwatakie kazi njema sana.
Abraham J. Mcharo
DUCE.