Na Baraka Mpenja,
Dar es salaam
MABINGWA watetezi
mara mbili mfululizo wa kombe la Mapinduzi, Azam fc wameanza vyema michuano
hiyo baada ya kuifunga Spice Stars mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi C jioni ya
leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Azam fc
yamefungwa katika dakika ya 71 kupitia kwa Mshambuliaji Mganda, Brian Umony
kufuatia kuwatoka mabeki wa Spice na kupiga mpira uliomshinda mlinda mlango,
Mohamed Silima.
Pasi ya bao hilo
litoka kwa kiungo mahiri wa Azam fc Salum Abubakar ‘Sure Bo”.
Bao la pili
lilifungwana na Himid dakika ya 86 kwa shuti kali, baada ya kuuwahi mpira
uliokuwa unaelekea mikononi mwa kipa Silima kufuatia shuti la Salum Abubakar.
Afisa habari wa
Azam fc ameuambia mtandao huu kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwani
wapinzani wao wameonekana kuwa imara.
“Tumeanza vizuri
kwa ushindi, lakini inaonekana michuano ya mwaka huu ni migumu sana. Spice
wameonesha upinzani mkubwa sana kwetu, lakini hatuwezi kusema lolote
kwani ni mapema sana”. Alisema Jafar.
Jafar aliongeza
kuwa kocha wao Mcameroon, Joseph Marius Omog anakisuka kikosi chao, hivyo
makosa yanayotokea yatafanyiwa marekebisho na kuhakikisha wanatwaa
ubingwa wao.
Aidha, Jafar kwa
niaba ya viongozi wa Azam fc amewapongeza vijana wao kwa kujituma na kupata
ushindi ambao haukuwa rahisi kabisa.
Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au
kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili usiku wa leo leo Uwanja
wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.
Kueleka katika
mchezo huo, wauza mitumba wa Ilala wamesema wapo tayari kuwamaliza wakenya.
Marijani rajab,
afisa habari wa Ashanti ameuambia mtandao huu kuwa kocha mkuu wa kikosi chao,
Abdalaah Kibaden Mputa amewapanga vijana wake kutokana na uzoefu wake katika
michuano mikubwa barani Afrika.
Katika mchezo
mwingine wa Kundi A, Uwanja wa Gombani, Pemba, URA ya Uganda imetoka sare
ya 2-2 na Chuoni ya Zanzibar.
Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule dakika ya 44 na 57, wakati ya Chuoni
yalifungwa na Shaaban Moke dakika ya 21 na Mwinyi Mngwali dakika ya 45
No comments:
Post a Comment