Hali ya mchezaji Joseph Owino wa Azam FC inaendelea vizuri kwa kufikisha asilimia 70 ya mazoezi ya viungo kujiweka sawa kabla ya kuanza mazoezi na timu ya wakubwa kamili kucheza mechi za ligi miezi miwili ijayo.
Owino alijiunga na Azam msimu huu akisumbuliwa na jereha la mguu wa kushoto, baada ya matibabu yupo katika mazoezi maalum ya viungo ili kurejesha mguu huo katika hali ya kawaida.
Akizungumza na www.azamfc.co.tz mwalimu wa viungo toka Ujerumani Paul Gomez amesema Owino hali yake inaendelea vizuri kadilii muda unavyokwenda amebakisha asilimia 30 kufikisha 100 ili kuwa kamili kwa kucheza mpira.
"Kutokana na tatizo lake anapata mazoezi ya viungo kwanza yatakayoufanya mguu wake urudi kama zamani na kuweza kuhimili kucheza na kukimbia bila kufanya hivyo mguu utamletea matatizo zaidi" Alisema Gomez.
Aliongeza kuwa baada ya kumaliza mazoezi ya viungo atajiunga na timu ndogo ya Azam Academy muda wowotekuanzia sasa kufanya mazoezi mepesi ya mpira wa miguu, endapo ataonekana kufanya vizuri atajiunga na timu kubwa na kuanza kucheza. kwa kuwa hatutaki kumharakisha tunatarajia itachukua miezi miwili lakini kama tungetaka kumharakisha tungeweza mtumia alisema Gomes.
Gomez alisema atafanya mazoezi na timu ndogo kwa muda ili kujenga uwezo wa kucheza na baadaye kurudi katika timu kwa ajili ya mechi za ligi kuu.
Owino alisajiliwa na Azam FC mwezi September mwaka jana, kabla ya kujiunga alikuwa mchezaji wa Simba SC.
Source: www.azamfc.co.tz
No comments:
Post a Comment