Search This Blog

Friday, November 9, 2012

WAKATI LIGI IKIFIKIA NUSU MSIMU - KAMATI YA LIGI IMELETA MABADILIKO GANI?? - AZAM NA KASUMBA ZA SIASA ZA SOKA - SIMBA UMOJA NDIO UDHAIFU WAO



Jumapili tutashuhudia mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom ukimalizika kwa timu mbalimbali zikijitupa uwanjani, sasa wadau wenzangu sijui tumejifunza nini na kuna tofauti gani na ligi ya mwaka jana au kuongezwa kwa nauli katika mkataba wa Vodacom kwa vilabu vya ligi kuu au kuondolewa kwa nembo ya mdhamini kifuani?


Vilabu vimenufaika na nini au mabadiliko gani yamefanyika kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko kulingana na hadhi ya ligi yenyewe?

 Ndio maana mimi tangu mwanzoni sikuwa muumini wa chombo kinachoitwa kamati na sababu ninazo. 

Tumeshuhudia ligi hii inayosimamiwa na kamati imeanza bila ya vilabu kusaini mkataba wa udhamini kutoka Vodacom kitu ambacho kikapelekea African Lyon kusaini mkataba na kampuni ya simu ya Zantel bila ya kujua kwamba katika mkataba wa Vodacom sehemu inayoeleza kuwa vilabu vinaweza kutafuta wadhamini lakini wasiwe washindani wa kibiashara na Vodacom na wana haki katika hilo pale African Lyon waliteleza kwa sababu umeshakubali kuolewa masharti ya ndoa uyafuate. 

Sasa basi sitaki kufika mbali dhamira yangu kwa wadau ni kueleza ni jinsi gani kamati haiwezi kutufikisha pale tulipotarajia kwa sababu ina watu wenye utashi zaidi katika mambo kama ya siasa, na mpira wa siku hizi ni sayansi na biashara sio siasa, sasa kama tutaendelea kuikumbatia kamati ya ligi tutakuwa tunafanya makosa sana nauliza swali kamati hii imefanya nini kuhakikisha vilabu vya ligi daraja la kwanza linachezwa kwa ufanisi?.


Madaraka achieni watu nyie endeleeni na siasa yenu kama kamati lakini pawe na chombo chenye wataalamu wa biashara, madalali wa kutafuta wadhamini mbona mambo yanawezekana lakini sisi tunataka mambo yote tuyafanye sisi eti kwa ajili kiongozi unakuta hapa katika mpira wetu mmoja ni Simba yeye, Yanga yeye, TFF yeye, chama cha mpira labda Rukwa yeye na kwenye kamati yeye, inakuwa unafiki, hivi vyeo vingine peaneni lakini ukweli ubakie palepale ligi yetu inahitaji kusimamiwa na watu wenye taaluma sio uzoefu.


 Kingine tumejifunza nini kwa timu yetu ya Azam nayo imejikita katika siasa, eti inamaliza ligi kwa staili ambayo ni aibu kwa timu kama Azam na siku za hivi karibuni ndio timu pekee niliyokuwa naitarajia itatoa somo matokeo yake ndio hivyo duuuh hii ni hatari jipangeni mmejaaliwa kila kitu hamna sababu ya kushindwa. Yanga nao walianza vibaya wamejipanga na Simba nao walianza vizuri lakini wametoka nje ya mchezo kwa sababu si wamoja.
Viongozi wa Simba SC
Lazima kuna namna, nimejaribu kufanya utafiti na kugundua kwamba uongozi wa samba samba sio collectively yaani wanafanya kazi kwa mafungu wapo kama kambale wote wana sharubu hajulikani jike wala dume yani mpaka mwanachama anaweza kusema Kaseja sio kipa!!!!! tuache uhuni tengenezeni umoja kwanza kwani utengano ni udhaifu, bila Simba imara Soka la kibongo litayumba, angalieni mlipojikwaa basi lakini jibu nimekupeni na mnalijua viongozi sio wamoja.

 Kuna mwandishi mmoja anaitwa J.K. Rowling, katika Harry Potter and the Goblet of Fire aliandika “We are only as strong as we are united, as weak as we are divided.” Mwisho namalizia na ndugu zangu wagombea wa DRFA jamani mkifukuza chizi ondoeni na makopo yake udambwi udambwi wa makato unaenda wapi mimi ndio maana sijachukua form nitaeleza maana yake nini wiki ijayo. 

Idd GodiGodi

No comments:

Post a Comment