WAKATI mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) baina ya Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan ukiingiza shilingi milioni 216,kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake ya mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa simu kutoka Visiwani Zanzibar ambapo timu imepiga kambi, msemaji wa Simba Ezeckiel Kamwaga alisema kwamba kikosi chao ambacho kimepiga kambi eneo la Mbweni kipo katika hali nzuri na kinafanya mazoezi katika uwanja wa Fuoni.
Aliongeza kuwa wamepania kushinda mchezo huo ili kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 na mahasimu hao katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambayo Simba inaongoza kwa pouinti 59 ikifuatiwa na Azam Fc yenye pointi 56 na Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46.
No comments:
Post a Comment