Shabiki wa soka ameripotiwa kuchomwa kisu mpaka kufariki baada ya kutokea majibizano juu ya matokeo ya mechi ya jana usiku ya premier league kati Man City and United iliyofanyika kwenye uwanja wa Etihad Stadium.
Mr.Stephen Ochieng Olouch, 24, ambaye ni mfanyabiashara wa biashara za kutembeza katika soko la Muthurwa, Nairobi, alichomwa kisu na ndugu yake baada ya kutokea kwa majibizano makali baada tu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa 1-0.
Kwa mujibu wa mdogo wa Ochieng Mercel Omondi, 22, ni kwamba kaka yake na ndugu yao walikuwa wanangalia mechi katika ukumbi wa Mbotela usiku wa jana na wakaanza kujibizana huku kila mmoja akitetea upande wa timu aliyokuwa akiishabikia.
Shahidi aliyeshuhudia tukio hilo amesema kwamba, "Wawili wale walikuwa wanakaa pamoja katika chumba cha kupanga - jana muuaji aliwahi kurudi kabla ya marehemu na kujifungua ndani. Marehemu Stephen aliporudi akagonga mlango kwa fujo huku akisema afunguliwe - alipofunguliwa mlango na mwenzie wakaanza tena kujibizana kitu ambacho kilipelekea wawili wale kushikana na kuanza kupigana kabla ya mtuhuiwa kuchukua kisu na kumchoma mwenzie kichwani."
Majirani hawakustuka kutokana na kelele za ugomvi ule kwa sababu wale jamaa kupigana na jambo la kawaida .
Mpaka sasa mtuhumiwa hajakamatwa na polisi wanaendelea kumtafuta.

No comments:
Post a Comment